TFA YAWAHAKIKISHIA WAKULIMA UPATIKAJI WA PEMBEJEO

 


Ferdinand Shayo ,Arusha.

Chama cha Wakulima Tanganyika (TFA) kimesema kuwa kitahakikisha wakulima ambao ni wanachama wa chama hicho wanapata huduma bora za pembejeo za gharama nafuu za kilimo ikiwemo mbegu na mbolea kupitia maduka ya chama hicho yaliyopo katika mikoa mbali mbali ya Tanzania.


Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa TFA uliofanyika Jijini Arusha ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TFA Waziri Barnaba amesema kuwa chama hicho kitaendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wake ili waweze kufanya kilimo cha kisasa chenye tija na kukuza uchumi wao kupitia kilimo.


Mkurugenzi Mtendaji wa TFA Jastin Shirima amesema kuwa chama hicho kitaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa wanachama wanafikiwa na mbolea za ruzuku kupitia matawi ya chama hicho yaliyotapaa kote nchini.

“Sisi kama TFA ni wadau wakubwa wa Wizara ya Kilimo na tunashirikiana nao kwa kwa karibu hususan katika suala zima la mbolea za ruzuku” Anaeleza Shirima.


Kwa upande wao Wanachama wa TFA akiwemo Elishilia Kimuto na Stanley Mwanri amesema wana Imani kubwa na chama hicho ambacho kimekua sauti kwa wakulima nchini na hususan katika suala zima la masoko ya uhakika kwa wakulima.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post