DKT. BITEKO AIPONGEZA EWURA KWA KUSHUSHA GHARAMA ZA UAGIZAJI MAFUTA




NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,akiipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kupitia upya gharama za uagizaji wa mafuta nchini leo Novemba 8,2023 wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa EWURA linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.


NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,akizungumza leo Novemba 8,2023 wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.



NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,akieleza jambo kwa washiriki wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.


NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).Dkt. James Andilile,akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa EWURA linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Rugemalira Rutatinwa Nyungwa,akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.


SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (hayupo pichani) , wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).Dkt. James Andilile,mara baada ya kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa EWURA linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kupitia upya gharama za uagizaji wa mafuta nchini kuwa zimekuwa rafiki kwa Taifa.

Dkt.Biteko ameyasema hayo leo Novemba 8,2023 wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa EWURA linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Dkt.Biteko amesema kuwa, awali zilikuwa kubwa na zilikuwa zikipelekea athari mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa gharama katika Sekta ya Usafirishaji na Uzalishaji.

“Gharama hizi za uagizaji mafuta zilikuwa kubwa mno huku kukiwa hakuna sababu ya kuwa kubwa kwa kiasi hicho, niliwapa maelekezo mkazitazame upya, nashukuru mmeziangalia na ninafurahi kwamba zimeshuka na hivyo kupunguza makali kwa watumiaji." Amesema Dkt. Biteko.

Aidha Dkt. Biteko amewataka Watendaji na Watumishi wa EWURA kuzingatia maslahi ya Watanzania katika kazi zao za Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ili Watanzania wapate huduma bora na kwa unafuu mkubwa.

“Tambueni kuwa Taifa lina mategemeno makubwa na ninyi, hivyo fanyeni kazi zenu kwa weledi na ubunifu mkubwa unaoendana na kasi ya teknolojia na maendeleo ya dunia; kanuni na miongozo yenu mnayotumia katika utekelezaji wa majukumu yenu''amesisitiza Dkt. Biteko

Hata hivyo amewataka Watumishi wa EWURA kuweka mkazo kwenye kudhibiti vitendo vya urasimu na rushwa mahali pa kazi, kutoangalia maslahi binafsi wakati wa kutenda kazi.

''Jiepusheni kuwaumiza Watanzania walio wengi,natoa wito kwa wafanyakazi hao kumkemea mtu yeyote anayeonekana kuwa na vitendo vya rushwa na ubinafsi katika eneo la kazi.''amesema

Pia amewataka Wafanyakazi wa EWURA kuwajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha kuwa watoa huduma wanafanya ushindani wenye tija na ufanisi wa kiuchumi, kulinda maslahi ya Walaji na mitaji ya kifedha ya Watoa Huduma.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt. James Andilile amesema kuwa uwepo wa Baraza hilo la wafanyakazi wa EWURA imekuwa kichochoe kikubwa cha maendeleo kutokana na ushirikiano wao katika mambo mbalimbali ikiwemo ushauri na maoni mbalimbali hasa katika bajeti ya kila mwaka ili kuweza kuboresha utendaji.

“EWURA inategemea sana uwepo wa baraza la wafanyakazi kwani wamekuwa ni watu muhimu sana ambao wametusaidia kutengeneza maono ya kuboresha utendaji hasa wa Menejimenti na watumishi mahali pa kazi,”amesema Dkt. Andilile

Naye Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Rugemalira Rutatinwa Nyungwa amesema kuwa ,Baraza la EWURA ni kati ya Mabaraza yanayojitahidi sana kutatua changamoto zinazowakabili Wafanyakazi na wanashirikiana vyema na Chama cha wafanyakazi na Muajiri ili kuhakikisha kunakuwa na utulivu mahala pa kazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post