DKT. KUSILUKA AIPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALIINa Sixmund Begashe -Dodoma 

Wizara ya Maliasili na Utalii imepongezwa kwa kazi nzuri ya usimamizi wa ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi awamu ya pili  la Wizara hiyo lililopo Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma, ambalo lipo tayari kwa matumizi ya Shughuli za kiofisi.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, alipolitembelea Jengo hilo kwenye ziara yake na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi unaondelea kwenye mji huo wa kipeke nchini. 

Aidha licha ya kuipongeza Wizara hiyo  Dkt. Kusiluka amehimiza ukamikishwaji wa kazi chache zilizobaki kwenye ujenzi huo.

Akizungumzia ujenzi wa Jengo hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi ameleza kuwa hadi sasa ujenzi wa jengo hilo umeshafikia asilimia 99% na kuwa asilimia Moja iliyobaki ni ya kazi ndogo ndogo za mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post