WAZIRI KAIRUKI KUJENGA KISIMA KATIKA SHULE YA KIBACHA WILAYANI SAME


Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 5, 2023 ambapo ameahidi kuwajengea Kisima cha maji kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji shuleni hapo.

***************

Na Happiness Shayo-Same

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameahidi kujenga kisima kikubwa cha maji katika Shule ya Sekondari Kibacha Wilayani Same, kwa lengo la kuendeleza kilimo cha mbogamboga na kuboresha lishe bora shuleni hapo.

Ameyasema hayo leo Oktoba 5, 2023 katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.

"Nimeguswa na ujumbe wa igizo la Watoto hawa kuhusu changamoto ya maji, naomba nitamke kuwa nitaijengea shule hii Kisima kikubwa cha maji ambacho pia kitawezesha kuendeleza kilimo cha mboga mboga na viazi lishe kwa ajili ya kuchangia lishe ya watoto wetu na hivyo kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha suala la lishe shuleni linapewa kipaumbele" Mhe. Kairuki amesisitiza.

Mhe. Kairuki amefafanua kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu na ilishaiona changamoto ya maji wilayani hapo hivyo, ipo kwenye hatua nzuri ya ukamilishwaji hadi kufikia mwaka 2024 Wilaya ya Same itakuwa na maji ya kutosha.

Aidha, ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za miradi mbalimbali ya elimu ili kuboresha sekta hiyo.

" Serikali kupitia Mradi wa Lipa kulingana na matokeo imetoa shilingi Billioni 7.5 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika Shule za Sekondari za Kidato cha Tano na Sita kote nchini."

Ameongeza kuwa Serikali pia imetoa shilingi Billioni 48 kujenga Shule za Wasichana za Bweni katika mikoa 16 Tanzania Bara na kupitia Mradi wa SEQUIP.

Katika hatua nyingine, Mhe. Kairuki amewaasa vijana wanaohitimu Kidato cha nne kuzingatia maadili ya Mtanzania na kuzingatia masomo.

"Vijana mnaohitimu Kidato cha Nne mwaka huu, mnapaswa kuelewa kuwa wazazi wenu na Taifa lina matarajio makubwa kutoka kwenu. Mnapaswa kuweka jitihada katika masomo yenu na kuwa na maadili mema kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu ma msijiingize katika maadili yanayofedhehesha utamaduni wetu ikiwemo ushoga na mengineyo." Mhe. Kairuki amesema.
Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiangalia maonyesho ya kisayansi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Kibacha akiwa ameongozana na uongozi wa shule pamoja na uongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same, kabla ya mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne ya Shule hiyo iliyopo, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 5, 2023.
Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi cheti Mhitimu wa Kidato cha Nne, Shabani Ibrahim katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 5, 2023. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibacha, Ngoka Manongi.
Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (wa pili kulia mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na wahitimu wa Kidato cha Nne katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 5, 2023. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni (kushoto), Katibu Tawala wa Wilaya ya Same, Upendo Wella (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Annastazia Tutuba (kulia)
Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa Wahitimu wa Kidato cha Nne mwenye changamoto ya ulemavu wa miguu, Naomi Mathayo katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 5, 2023.
Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (katikati) akifuatilia matukio katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 5, 2023. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni na kushoto kwake ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibacha, Ngoka Manongi.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibacha, Ngoka Manongi akitambulisha baadhi ya wageni walioshiriki Mahafali ya saba ya Shule ya Sekondari Kibacha, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 3,2023. Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni.
Baadhi ya washiriki wa mahafali ya saba ya Kidato cha Nne ya katika Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wakifuatilia matukio katika mahafali hayo yaliyofanyika leo Oktoba 5, 2023.
Baadhi ya wazazi , ndugu, jamaa na marafiki wa wanafunzi waliohitimu Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wakifuatilia matukio katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne ya shule hiyo yaliyofanyika leo Oktoba 5.
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb)(hayupo pichani) akizungumza katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro yaliyofanyika leo Oktoba 5.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post