DANIEL NOBOA ASHINDA URAIS ECUADOR, NDIYE RAIS MWENYE UMRI MDOGO ZAIDI


Mfanyabiashara Daniel Noboa anatarajiwa kuwa rais mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Ecuador, akiwa na umri wa miaka 35.

Bw Noboa alishinda uchaguzi wa Jumapili kwa 52.3% ya kura, mbele ya Luisa González 47.7%.

Alikubali kushindwa na kumpongeza mpinzani wake. Mzee huyo mwenye umri wa miaka 35, wa chama cha National Democratic Action, ni mtoto wa Álvaro Noboa, ambaye aligombea urais mara tano bila mafanikio.

Bw Noboa atakuwa na miezi 17 pekee madarakani hadi uchaguzi ujao.

Atatawala kuanzia mwisho wa Novemba 2023 hadi Mei 2025, kwa sababu uchaguzi wa sasa ulianzishwa mapema wakati Rais anayemaliza muda wake Guillermo Lasso alivunja bunge huku kukiwa na kesi ya kumuondoa madarakani.

Anaweza kuwania tena muhula wa urais wa 2025-29 ikiwa anataka.

Bw Noboa ataapishwa kuwa rais tarehe 25 Novemba, siku tano kabla ya kutimiza miaka 36.

Kufuatia ushindi wake katika duru ya pili ya upigaji kura, Bw Noboa aliwaambia wafuasi wake: "Kesho tunaanza kazi ya Ecuador hii mpya, tunaanza kufanya kazi ya kujenga upya nchi iliyoathiriwa vibaya na ghasia, ufisadi na chuki."

Ecuador imekumbwa na ongezeko la ghasia za magenge katika miaka ya hivi karibuni na kampeni ya urais ilikumbwa na mauaji ya mwezi Agosti ya mgombea Fernando Villavicencio.

Chanzo - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post