AJALI YA BOTI YAUA WATU 30 MTO KONGO


Picha na Maktaba
 **
Takriban watu 30 wanasadikiwa kufa maji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya boti kuzama katika Mto Kongo.

Kuna hofu kuwa huenda idadi ya waliopoteza maisha ikaongezeka huku juhudi za utafutaji na uokoaji zikiendelea.

Zaidi ya watu 160 bado hawajulikani walipo kutokana na ajali ya boti iliyotokea Ijumaa karibu na Mbandaka kaskazini-magharibi mwan nchi.

Ripoti zinaonyesha boti hiyo, ambayo ilikuwa ikisafiri usiku kwa kukiuka kanuni, huenda ilikuwa na abiria wengi kupita kiasi.

Maafisa wanasema ilikuwa imebeba zaidi ya watu 300 pamoja na mizigo, ikiwa ni pamoja na saruji, mafuta na chuma.

Kutokana na ukosefu wa mtandao wa kitaifa wa barabara, usafiri wa mto hutumiwa sana nchini DR Congo, na ajali hutokea mara kwa mara.

Chanzo - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post