EWURA SACCOS YAPEWA CHANGAMOTO KUONGEZA WANACHAMAMwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu, Mha. Poline Msuya, ambaye ni Mkurugenzi wa Gesi Asilia EWURA, akifungua Mkutano wa Nne wa EWURA SACCOS , jijini Dodoma leo 9 Septemba 2023

Na.Mwandishi Wetu-DODOMA

Chama cha Akiba cha Kuweka na Kukopa cha wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA SACCOS) kimetakiwa kuhakikisha kinaongeza idadi ya wanachama ili kuendelea kukiimarisha na kukuza mtaji wake mwaka hadi mwaka kwa lengo la kuongeza wigo wa kuhudumia wanachama ili waweze kuboresha maisha yao.

Mha. Poline Msuya, aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa EWURA katika Mkutano huo, ametoa rai hiyo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nne wa EWURA SACCOS uliofanyika jijini Dodoma leo, 9 Septemba, 2023.

“Natamani kila mfanyakazi wa EWURA awe mwanachama wa EWURA SACCOS, hivyo nitumie fursa hii kutoa rai kwa viongozi wa Chama, kuainisha mbinu na mikakati ya kuhamasisha wafanyakazi kujiunga ili kuchochea maendeleo ya SACCOS na kuimarisha uchumi wao” Alisisitiza.

Mwenyekiti wa EWURA SACCOS, Mha. Titus Safari, alieleza mafanikio ya SACCOS hiyo, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020, kuwa ni kuongezeka rasilimali zake kutoka mil 200 hadi milioni 700; kuweka mfumo wa kieletroni wa kumbukumbu za wanachama, kuongezea idadi ya wanachama kutoka 98 hadi 122 na kupata hati safi ya ukaguzi wa mahesabu kwa miaka mitatu mfululizo.

Naye Meneja wa SACCOS, Bw. Victor Chiwanga, alieleza kuwa, Chama hicho kimejipambanua na kujizatiti kukuza mtaji tete wake kwa kuongeza thamani ya hisa na idadi ya wanachama kwa mujibu wa kanuni zake.

Uchaguzi wa viongozi mbalimbali ulifanyika wakati wa mkutano huo ambapo Mha. Titus Safari alichaguliwa kwa mara nyingine kwenye nafasi ya Uenyekiti, huku Bw. Benjamin Beda akiendelea kuwa Makamu Mwenyekiti.

Viongozi wengine waliochaguliwa ni Bi. Rahel Kiula, Bw. Jerome Kipesha na Bi. Mariam Naah, wanaounda Kamati ya Usimamizi ya Chama na watadumu kwa kipindi cha miaka mitatu ( 2023-2026).

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu, Mha. Poline Msuya, ambaye ni Mkurugenzi wa Gesi Asilia EWURA, akifungua Mkutano wa Nne wa EWURA SACCOS , jijini Dodoma leo 9 Septemba 2023

Baadhi ya Wanachama wa EWURA SACCOS wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Nne wa Mwaka jijini Dodoma leo 9 Septemba 2023
Picha ya pamoja ya wanachama wa EWURA SACCOS baada ya kushiriki Mkutano Mkuu wa Nne, jijini Dodoma leo 9 Septemba 2023

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post