WALIMU WATAKIWA KUTUMIA BENKI YA NMB KUJIKWAMUA KIUCHUMI

MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akizungumza wakati alipomwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema  katika kongamano la siku ya  Walimu wa Mkoa wa Tanga lililoandaliwa na Benki ya NMB na kufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini humo.
MKUU wa Kitengo cha Bima wa Benki ya NMB Makao Makuu Martin Massawe akizungumza wakati wa kongamano la siku ya Walimu wa Mkoa wa Tanga lililoandaliwa na Benki ya NMB na kufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini humo na kufunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Ladislaus Baraka akizungumza wakati wa kongamano la siku ya Walimu wa Mkoa wa Tanga lililoandaliwa na Benki ya NMB na kufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini humo na kufunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji,ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema

Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kongamano la siku ya walimu wa Mkoa wa Tanga lililoandaliwa na Benki ya NMB na kufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini humo na kufunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema
sehemu ya Walimu kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Tanga wakifuatilia kwa umakini Kongamano la siku ya walimu wa Mkoa wa Tanga lililoandaliwa na Benki ya NMB na kufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini humo na kufunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji, ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyemaha
sehemu ya Walimu kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Tanga wakifuatilia kwa umakini Kongamano la siku ya walimu wa Mkoa wa Tanga lililoandaliwa na Benki ya NMB na kufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini humo na kufunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji, ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema

 Na Oscar Assenga, TANGA.

MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji amewataka walimu mkoani humo kuhakikisha wanaitumia benki ya NMB kutokana na bidhaa zao wanazotoa za mikopo ambazo zimeweza kuwainua kimapato na hatimaye kuwakwamua kiuchumi badala ya kujiingiza kwenye mikopo kandamizi.

Kaji aliyasema hayo wakati alipomwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema  katika kongamano la siku ya  Walimu wa Mkoa wa Tanga lililoandaliwa na Benki ya NMB na kufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini humo.

Ambapo alisema kwamba hilo ni kutokana na kwamba benki hiyo kusheheni huduma mbalimbali ambazo wanaweza kuzitumia katikaa kujikwamua kiuchumi na kuondokana na mikopo kandamizi.

“Niwapongeza NMB kwa kuandaa Kongamano hili kwa walimu ni ya kipekee kwani nimetoa msisitizo kwa kutumia nguvu nyingi kuwezesha walimu kwenye shule za Msingi na Sekondari kwani wamekuwa wakiishi kwenye mazingira magumu  kutokana na kujiuingiza kwenye mikopo umiza”Alisema

Aidha alisema mikopo hiyo imekuwa ikiwaumiza na hivyo kupelekea kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kuweza kufundisha kutokana na kutumia muda mwingi kufikiria namna ya kuirejesha.

“Warsha hii imekuja wakati muafaka na niipongeza NMB nitoa wito kwa walimu kuweza kutumia NMB kutokana na bidhaa zao wanazotoa za mikopo ambapo lakini tumeshuhudia jinsi benki ilivyoweza kuwainua kimapato na kuweza kuboresha maisha yao hali inayoongeza uwezo kwenye utumishi wa kazi zao za kila siku”Alisema

Awali akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya NMB Makao Makuu Martin Massawe alisema kwamba wamezindua mpango maalumu kwa ajili ya walimu ambao waliuita “Specho” na wamekuja Tanga kutoa elimu zaidi na kusisitiza juu ya huo mpango unaomwezesha mwalimu kupata mikopo yenye riba nafuu ikiwemo ya kujiendeleza kielimu wao na watoto wao.

Alisema pia wanatoa mikipo ya biashara ndogo ndogo ,ujenzi,vyombo vya moto kama bodaboda na pikipiki za miguu mitatu ikiwemo kupata mkopo wa bima yaani Insurance Premium Finance (IPF) ambayo inawezesha walimu kulipa bima kujikinga na majanga mbalimbali.

“Lakini pia tunatoa mikopo ya pembejeo na mashine za kilimo fursa za kushiriki promosheni na kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo elimu ya kifedha kwa walimu na kadhalika”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba Tafiti zinaonyesha kati ya watanzania milioni 60,ni asilimia 22 tu ndio wenye akaunti za benki pia zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wanaamiliki simu za mkononi na wana uwezo wa kufanya malipo na miamala kupitia simu zao za mkononi.

“Kwa kulitambua hilo benki yenu ya NMB imeendelea kuja na masuhulisho mbalimbali yanayohusu makundi tofauti tofauti kama hili la walimu kama njia mojawapo ya kuleta watanzania zaidi kwenye mifumo rasmi ya kifedha na kuipatia Serikali mapato kupitia masuluhisho hayo pia benki imeweza kufikishja asilimia 94 ya miamala yake kupitia simu za mkononi”Alisema

Hata hivyo alisema hivi karibuni wamezindua huduma kubwa tatu ambazo zinaendelea kuleta mapinduzi makubwa katika sekta hya kibenki Tanzania ambazo ni mikopo kidigitali (MshikoFasta),NMB Pesa Wakala na NMB Lipa Mkononi.

Alisemna kupitia mifumo hiyo wameweza kuwafikia watanzania wengi zaidi na hivyo kuchangia kuongeza idadi ya watanzania wanaotumia huduma za kibenki na pia hata kuwasaidia walimu ambao wanaweza wakawa mbali na matawi ya benki.

Naye kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Ladislaus Baraka alisema siku ya mwalimu kwa benki ya  NMB ilianzia mkoa wa Tanga miaka ya nyuma wilaya ya Korogwe kwa zaidi ya miaka 7 iliyopita na wameendelea kuboresha huduma zao.

Alisema  kwa sababu walimu wameendelea nao wafanye nini na niwashukuru walimu mmekuwa wateja wote wa thamani sana kutokana na walimu kuwa chachu kubwa kwao kubioresha huduma zao wanazotoa kwa mikopo na hudumaza bidhaa mbalimbali na mwaka 2005 walikuwa wanaliopa mishaha kupitia madirisha yaliyokuwa halmshauri na baada kupitia benki .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post