AJINYONGA KISA UGUMU WA MAISHA AKIUMWA MACHO NA KIUNO TINDENa Halima Khoya, Shinyanga.

Mwanaume aitwaye Muhangwa Swila (56) mkazi wa kitongoji cha Mwandu Kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga Mkoa wa Shinyanga, amekutwa amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani chanzo kikidaiwa kuwa ni ugumu wa maisha akisumbuliwa na maradhi ya macho, kiuno na mgongo.

Akizungumza na Malunde 1 Blog Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga,ACP Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea  Agosti 8, 2023 majira ya saa sita usiku ambapo walimkutwa Muhangwa Swila akiwa amejinyonga juu ya mti karibu na nyumba yake.

Magomi amebainisha kuwa Swila alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya macho,mgongo na kiuno ambapo amesema hizo hazikuwa sababu za kifo chake na kwamba mwili wake ulifanyiwa uchunguzi kisha kukabidhiwa kwa ndugu kwaajili ya taratibu za mazishi.

“Muhangwa Swila hajaacha ujumbe wowote,bali kutokana na uchunguzi wa kiintelijensia tumegundua alikuwa akisumbuliwa na macho, mgongo, na kiuno lakini kubwa zaidi ni ugumu wa maisha kwa hiyo alikuwa anajikataa huenda ikawa sababu kuu ya kujiua”, amesema Magomi.

“Natoa wito kwa wananchi, habari ya ugumu wa maisha isiwe sababu ya kuchukua hatua za kupoteza uhai,hospitali zipo nyingi,ukiwa na changamoto yoyote jitahidi uwahi kutibiwa”, ameongeza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post