Picha : MADIWANI WAWASILISHA TAARIFA ZA KATA... "MANISPAA YA SHINYANGA INA UPUNGUFU WALIMU WA KIUME, WATENDAJI... MWAMALILI HAWANA KABISA UMEME"

Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendelea

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amesema Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ina upungufu mkubwa wa walimu hasa walimu wa kiume hivyo kuiomba serikali kuangalia namna ya kutatua changamoto hiyo.

Masumbuko ametoa ombi hilo leo Jumatano Agosti 9,2023 wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Shinyanga kilichokuwa na ajenda ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa shughuli mbalimbali kutoka katika kata kwa robo ya nne yam waka 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
“Manispaa yetu ina upungufu mkubwa wa walimu hasa walimu wa kike, unakuta kuna shule ina walimu 13 lakini mwalimu wa kiume mmoja pekee. Tunaomba kuongezewa walimu na kuwe na uwiano wa walimu wa kiume na wa kike kwani wanafunzi wa kiume wana mahitaji mengine yanapaswa kusikilizwa na walimu wa kiume na wanafunzi wa kike nao wanahitaji kusikilizwa na walimu kike”,amesema Meya huyo wa Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko.

Aidha ameliomba Jeshi la polisi kuchukua hatua kwa waendesha pikipiki wanaokiuka kanuni na sharia za usalama barabani ikiwemo kupakia mizigo mikubwa kuzidi kiasi na kuathiri watumiaji wengine wa barabara.

“Polisi tunaomba bodaboda wanaopakia mbao mchukue hatua kwa sababu kuna malalamiko pikipiki zinachukua nafasi kubwa sana barabarani lakini zinabeba mzigo mkubwa juu ya kiwango kinachotakiwa”
,amesema Masumbuko.

Kuhusu malalamiko ya wananchi yaliyowasilishwa na  Diwani wa kata ya Mwamalili James Matinde juu ya kukosekana kwa huduma ya Umeme kwenye kata yote, Meya huyo amesema suaala hilo linashughulikiwa , Mkandarasi amepatikana na hivi karibuni huduma ya umeme itapelekwa kwenye vijiji vyote vitatu vya kata hiyo.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga amewataka Madiwani kutilia mkazo suala la Lishe shuleni huku akihamasisha ujenzi wa vyoo kwenye baadhi ya shule ikiwemo shule ya Sekondari Uzogore zenye upungufu wa matundu ya vyoo kwani kukosekana kwa vyoo kunafanya utu ukosekane.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga ambaye ni Mwanasheria Dorice  Dario amesema juhudi za serikali zinafanyika ili kuweza kupata watumishi wakiwemo maafisa watendaji na suala la shule ikiwemo Uzogore Sekondari linashughulikiwa haraka na liliwekwa kwenye mpango wa bajeti wa mwaka wa fedha huu.

Licha ya mafanikio yaliyofikiwa kupitia kikao hicho, Madiwani wamezitaja miongoni mwa changamoto zilizopo ni upungufu wa madarasa, uhaba wa matundu ya vyoo, kukosekana kwa huduma ya maji katika baadhi ya shule, upungufu wa maafisa watendaji ,ukosefu wa umeme kwenye baadhi ya maeneo mfano kata ya Mwamalili ambayo vijiji vyote havina umeme na upungufu wa walimu kwenye baadhi ya shule.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Jumatano Agosti 9,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga  
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga ambaye ni Mwanasheria Dorice  Dario akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga ambaye ni Mwanasheria Dorice  Dario akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendelea

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post