MCHUNGAJI MTATA ATANGAZA MAJI YA UPAKO WA UTAJIRI.. "UNAKUNYWA AU KUOGA UNAPATA GARI"


Mhubiri maarufu nchini Kenya Victor Kanyari sasa anasema amepata dawa ya kukabiliana na umaskini.

Mchungaji huyo wa kanisa la Salvation Healing Ministry alinaswa kwenye video akizungumzia kuhusu maji maalum ambayo alidai yakitumiwa humfanya mtu kuwa tajiri, akiunga mkono hadithi yake na andiko la Biblia.

Alisema alipata gari la KSh 15 milioni na mengine mengi kutokana na maji. Mhubiri huyo alidai zaidi kwamba alimsaidia mjakazi ambaye alitii shauri lake la kuoga kwa maji mahsusi na kupata utajiri mara moja.

"Unapooga na hii na huna pesa mara moja inaanza kuja. Ninakuambia kuwa nimebarikiwa. Gari hili ni KSh 15 milioni, na ninazo nyingi. Kuna mwanamke mmoja ambaye alifanya kazi ya ujakazi. Nilimpa maji haya akaoga nayo akaacha kazi na kununulia gari atatupa ushuhuda,” alisema.

Kanyari wa umaarufu wa "mbegu ya 310 " anayehusishwa na sarakasi za kimiujiza alijenga bwawa kanisani mwake kuwaponya waumini.

Hivi majuzi aliweka bomba na bwawa la maji ndani ya kanisa lake. Katika video nyingine isiyo na tarehe iliyowaacha watu mitandoani wakiwa wameduwaa, kasisi huyo alifichua kuwa kisima hicho kitaitwa Bethsaida. 

Kanyari anayejulikana kwa tabia zake zisizo za kawaida, alionekana akimshauri mmoja wa wafuasi wake kunywa na kuoga kwa maji hayo. Kulingana naye, maji hayo yana uponyaji na miujiza yenye uwezo wa kutatua shida za watu zote.

"Nawa mikono, unaweza hata kuoga kisimani ukipenda. Kunywa kidogo pia. Sasa matatizo yako yamekwisha," alimwambia msichana mmoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post