BUSHAKO : VIJANA WA CCM MSIKUBALI KUTUMIWA NA WANASIASA TUEPUKE MATABAKA CCMMakamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Muleba, Bw. Muhaji Bushako
****

Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera wametakiwa kuepuka kutumiwa na wanasiasa kwenye maeneo yao ili kuepusha   kuwepo kwa matabaka kwenye jumuiya hiyo.


Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Muleba, Bw. Muhaji Bushako amesema hayo  kwenye kikao cha baraza la Umoja wa Vijana  wa Chama cha Mapinduzi cha Wilaya cha kikanuni kwa  mwezi wa sita  ambapo amesema kuwa vijana wanao wajibu wa kuhakikisha wanajisimamia wenyewe.

Bushako amesema wapo baadhi ya vijana wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa kwenye maeneo yao na kusababisha kuwepo kwa matabaka hivyo wanalo jukumu la kuhakikisha wanajisimamia na kuwa kitu kimoja kwani  jumuiya hiyo ni tanuru ya uongozi.

 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Muleba Bwana Geofrey Kamili amewataka vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi  katika  uchaguzi wa Serikali za mitaa  kwenye maeneo yao ambao unatarajia kufanyika hapo mwakani kwani  jukumu la kuwa kiongozi sio la watu wazima pekee.

Nao baadhi ya wajumbe wa balaza hilo la Vijana ambao ni Minath Mickdard na Muksini Mohamed wamesema kuwa kitendo cha kutumika ki siasa kina athiri maendeleo ya jumuiya hiyo ambapo watahakikisha wanakuwa wamoja na kuondoa matabaka kwenye jumuiya hiyo.

Aidha katika kikao hicho wajumbe walimpitisha katibu hamasa wa Jumuiya ya vijana CCM wilaya ya Muleba Mohamed Isumail Rwabakoba.
Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Muleba, Bw. Muhaji Bushako

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post