TASAC WASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA BIASHARA YA SABASABAAFISA Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin akitoa elimu kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye Banda lao katika Maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam

 Mwananchi aliyetembelea Banda la TASAC akipatiwa zawadi katika Banda la TASAC

Watumishi \wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wengine wa Shirika hilo wakiwa kwenye Banda laoNa Mwandishi Wetu,Dar es Saalam

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania, TASAC linashiriki katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa.

Maonesho hayo yenye Kauli Mbiu “Tanzania Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji”, yameanza tarehe 28 Juni, katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam na yatahitimishwa tarehe 13 Julai , 2023.

Akizungumza leo Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika hilo Martha Kelvin alisema lengo la kushiriki maonesho hayo ni kujenga uelewa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi na majukumu yanaotekelezwa na TASAC kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415 na mabadiliko yake.

Hata hivyo alisema kwamba TASAC inawaalika wananchi wote kutembelea maonesho haya na kufika katika banda la TASAC lililopo katika ukumbi wa Karume banda namba 22 na 23.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post