NAIBU KATIBU MKUU UJENZI AFUNGUA KIKAO CHA FARAGHA CHA BODI YA MFUKO WA BARABARA SINGIDA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Ludovick Nduhiye, akihutubia Menejimenti na Wafanyakazi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (hawako pichani), kwenye kikao cha faragha cha Bodi hiyo kinachofanyika kwa siku mbili mkoani Singida.

Kaimu Meneja Mfuko wa Barabara Mhandisi Rashid Kalimbaga, akisoma taarifa yake kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Ludovick Nduhiye (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa kikao cha faragha cha Bodi hiyo kinachofanyika kwa siku mbili mkoani Singida.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Xavier Daudi, akiongelea Suala la kuimarisha ari na morali kwa watumishi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara katika utekelezaji wa majukumu yao ya kiutumishi. Aliyeketi kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi wa Bodi hiyo Abdallah Mtey.Baadhi ya Watumishi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Ludovick Nduhiye, wakati akifungua Kikao cha Faragha cha Bodi hiyo kinachofanyika kwa siku mbili mkoani Singida.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi) Ludovick Nduhiye (aliyeketi katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, baada ya kufungua kikao cha faragha cha Bodi hiyo kinacho fanyika mkoani Singida. Kulia kwa Nduhiye ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Xavier Daudi, kulia kwake ni Kaimu Meneja Mfuko wa Barabara Mhandisi Rashid Kalimbaga, Wengine ni Meneja Msaidizi Utawala na Fedha wa Bodi John Aswile (kulia) na Meneja Msaidizi Mapato wa Bodi Godlove Stephen (Kushoto).

Picha na Bodi ya Mfuko wa Barabara

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post