CHONGOLO AWASILI JIJINI MWANZA KUFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA


******************

Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo amewasili leo Julai 30,2023 katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza tayari kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.

Baada ya kuwasili Katibu Mkuu Chongolo amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wa Mkoa huo.

Katika mkutano huo maalum wa hadhara unaotarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wanaCCM na wananchi kwa ujumla, kutoka mkoa huo na mikoa mingine ndani ya Kanda ya Ziwa, Komredi Chongolo na ujumbe wake wataelezea na kufafanua hatua kwa hatua kuhusu uamuzi wa Serikali kuingia makubaliano ya uwekezaji wa kuboresha uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, lengo likiwa kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma kwa ufanisi mkubwa tofauti na ilivyo sasa, ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 - 2025.

Katibu Mkuu huyo wa CCM ameambatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Stephen Wasira, Katibu wa NEC Oganaizesheni Usi Gavu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Ndugu Kitila Mkumbo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Mhe. Jerry Silaa pamoja na Wakili Msomi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albert Msando.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments