VIJANA 182 WAPIKWA KUTUMIKIA JESHI LA JADI SUNGUSUNGU ITWANGI, RPC MAGOMI ATAKA WAZINGATIE MAADILI


Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akizungumza kwenye Mkutano wa Sungusungu katika Kijiji cha Imenya Kata ya Itwangi,ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Itwangi Kamuli Makomango akizungumza kwenye Mkutano wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Itwangi Halmashauri ya Shinyanga wakati wa kufunga mafunzo kwa vijana 182 kutoka Vitongoji vya Imenya na Igomelo Kata ya Itwangi ambao wameingizwa rasmi Jeshi la jadi Sungusungu.


Na Elias Gamaya - Shinyanga 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi amelitaka Jeshi la jadi maarufu Sungusungu kutoka Vitongoji viwili vya Imenya na Igomelo Kata ya Itwangi kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwemo kujiepusha na vitendo vya kihalifu.


Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya mwezi mmoja ya vijana 182 ambao wameingia katika Jeshi la jadi Sungusungu rasmi ili kusaidia kudhibiti wahalifu wiki iliyopita, Kamanda Magomi amewasihi kuzingatia sheria na kuacha kujichukulia sheria mkononi badala yake wawafikishe polisi.

"Jeshi la jadi lipo kisheria kupitia sheria ya Mgambo na linatambulika kisheria na lilianza kupata umaarufu, sisi Jeshi la Polisi hatutoshi kama polisi mmoja anatakiwa kulinda raia 450 tu katika suala zima la ulinzi na usalama lakini kinachotokea sasa kutokana na uchache wetu askari mmoja analinda raia 1700”, amesema Kamanda Magomi.
Kamanda Magomi amesema Mkoa wa Shinyanga bado unakabiliwa na mauaji,ndoa za utotoni, mimba kwa wanafunzi,ubakaji,kulawiti na baadhi ya watu kujihusisha na mapenzi ya ndoa za jinsia moja mambo ambayo yanatakiwa kukemewa katika jamii ili kukomesha vitendo hivyo.


Awali akielezea historia ya Jeshi la Jadi Muelimishaji ambaye pia ni Mhasibu wa Tarafa ya Itwangi, Philipo Malongo amesema kabla ya kuitwa jeshi la jadi lilikuwa linaitwa shirika la kurudisha mali za watu ikiwemo mifugo kutokana na kukithiri kwa matukio ya wezi wa mifugo kwa kipindi cha mwaka 1981.

Amesema malengo na madhumuni ya Jeshi hilo ni kuwaelimisha vijana ili waielewe sungusungu,kuawezesha vijana kubadilika na kuwafundisha nidhamu vijana ambapo mafunzo hayo hufanyika kila baada ya miaka mitano.


“Sungusungu haikuwekwa kwa ajili ya kuwatesa vijana bali iliwekwa kwa nia ya kuwafundisha kuwa na nidhamu na kuwatengeneza kuendana na kanuni na sheria za nchi yetu”,amesema Malongo

Nao baadhi ya sungusungu wa jeshi hilo wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kukabiliana na wahalifu,pia kusaidia kupunguza vitendo vya kihalifu ili hatua za haraka zichukuliwe kukabiliana na matukio hayo na kuyakomesha.
Sungusungu wakiwa kwenye Mkutano
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Mwezeshaji wa mafunzo kwa vijana walioingizwa rasmi Jeshi la jadi Sungusungu Tarafa ya Itwangi Philip Malongo akizungumza kwenye Mkutano
Diwani wa Kata ya Itwangi Sonya Jilala akizungumza kwenye Mkutano wa Sungusungu
Mkutano unaendelea
Mkutano wa Sungusungu unaendelea
Viongozi wakifuatilia Mkutano

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post