MWALIMU AWAPA MIMBA WANAFUNZI WAWILI, NYINGINE ATOA

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Paulo Chacha ameagiza kukamatwa kwa walimu wawili na mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi kilimo kata ya Ukiliguru, baada ya mwalimu mkuu wa shule hiyo Charles Maige, kutuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wake wa darasa la saba.

Mwalimu huyo anakabiliwa na tuhuma nyingine za kumtoa mimba mwanafunzi mwingine aliyekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi, ili kukwepa mkono wa sheria, ikiwa ni pamoja na kuendelea kujihusisha na mahusiano ya namna hiyo na wanafunzi wengine wawili wa darasa la saba.

Mwalimu mwingine aliyetiwa mbaroni ni Venance Komba, anayedaiwa kumshawishi mwanafunzi huyo mwenye ujauzito (jina limehifadhiwa), kushiriki naye kimapenzi, huku akimtisha kufichua siri ya uhusiano wake na mwalimu mkuu wa shule hiyo Charles Maige, iwapo hatakubaliana na ushawishi huo.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Misungwi Paulo Chacha, inadaiwa kwamba mtoto huyo mwenye umri wa miaka 16 asiyekuwa na wazazi alisitisha masomo kutokana na kupata ujauzito.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post