GGML YAELIMISHA WADAU UTEKELEZAJI MPANGO WA CSR

MAONESHO ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam, yanayofanyika katika viwanja vya SabaSaba jijini Dar es salaam yamekuwa ni fursa adhimu kwa wadau mbalimbali kushuhudia namna kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) inatekeleza Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).


Moja ya wadau hao ni Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse ambaye juzi Jumanne tarehe 4 Julai 2023 ametembelea banda la GGML katika maonesho hayo yanayoendelea jijini Dar es Salaam.


Dk. Mwasse alipata maelezo kutoka kwa Afisa Manunuzi (Mikataba) wa GGML, Silas Shija (wa kwanza kulia) aliyekuwa ameambatana na Scholastica Hoya, Ofisa Rasilimali Watu na Innocent Mushi ambaye ni Ofisa Mwandamizi (Rasilimali Watu).

Walieleza jinsi GGML inavyosaidia miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi katika jamii zinazozunguka migodi yake kama vile elimu, afya, maji, miundombinu na kilimo.

Miradi hii inaakisi dhamira ya GGML kwa jamii inayozunguka mgodi kuwa na maendeleo endelevu.

Mojawapo ya maadili yake ya msingi, na maono yake ni kutoa mchango chanya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post