RC FATMA MWASSA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA KUTOKA CONGO


Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa (katikati) akiwa na wafanyabiashara kutoka Congo
Wafanyabiashara kutoka Congo
Nichoulas Basimaki mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Kagera

Na Mariam Kagenda _ Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa amekutana na wafanyabiashara wa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliofanya ziara Nchini Tanzania mkoa wa Kagera kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kibiashara.

Akizungumza na wafanyabiashara hao katika ukumbi wa Ofisi yake Mhe. Mwassa ameeleza juu ya fursa mbalimbali za uwekezaji wa biashara zilizopo Mkoa wa Kagera, ikiwemo ujenzi wa maghala ya kuhifadhi chakula, ujenzi wa hoteli za kitalii, ujenzi wa machinjio ya kisasa na viwanda vya nyama, uuzaji wa dagaa nje ya Nchi, ufugaji wa ng’ombe, ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba na kilimo cha mazao mbalimbali kama kahawa.

“Kama nilivyowadokeza, Mkoa wetu wa Kagera na Tanzania kwa ujumla tunavyo vivutio vingi na fursa nyingi za biashara katika mazao ya samaki katika Wilaya za Bukoba, Missenyi na Muleba. Lakini pia tunayo maeneo ya kutosha kwa ajili ya maeneo ya kilimo biashara na ufugaji wa ng’ombe,” ameeleza Mhe. Mwassa

Amesisitiza juu ya ushirikiano wa kibiashara kati ya wafanyabiashara hao na wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera
 kutumia mazingira rafiki ya uwekezaji kwa kuzingatia Mkoa wa Kagera ulipo kijiographia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ndg. Joyeux Bahidika amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano walioupata kwa kuwapa nafasi ya kuja kujifunza na kuona fursa za uwekezaji katika Mkoa wa Kagera. Huku akimuahidi kuendelea kushirikiana katika sekta hiyo ya biashara.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Kagera, Ndg. Nichoulaus Basimaki kuwa wanayo matarajio makubwa sana kufanya biashara na wafanyabiashara wa Congo kutembelea fursa mbalimbali zilizopo. Kama wafanyabiashara wamejiandaa kwenye maeneo ya mnyororo wa thamani.

Aidha yapo mazao ya samaki ambayo wamekuwa wakifanya biashara wa Nchi ya Demokrasia ya Congo tayari wameshamasisha wafanyabiashara wamefungua makampuni na wapo tayari kufanya biashara, hivyo wapo tayari kutekeleza mazimio na mkataba waliokubaliana mwezi April, 2023 kati ya Jimbo la Kivu Kusini, Congo na Nchi ya Tanzania Mkoa wa Kagera.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post