MCCCO YAKOBOA TANI 18,875 ZA KAHAWA

 

Picha za mashamba ya kahawa ya  wakulima katika kijiji cha Langilo kata ya Langilo bonde la Hagati Maguu wilaya ya mbinga Ruvuma.

Na Mwandishi wetu

Kiwanda cha kikuu cha wakulima wa zao la kahawa wilaya ya mbinga mkoani  Ruvuma MCCCO LTD MBINGA COFFEE CURING  kwa msimu wa mwaka 2022/2023 kimefanikwa kupokea kahawa na kukoboa kutoka kwa wakulima zaidi ya tani 18, 875 kati ya tani 18000 ya uzalishaji wote ambapo tani zilizosalia zilichukuliwa na viwanda vingine vinavyo jihusisha na ukoboaji.


Akiongea na Gazeti la Kilimo ofisini kwake Meneja mkuu wa kiwanda hicho Festo Chang'a amesema kuwa kiwanda hicho kina kutana na changamoto nyingi za upokeaji kahawa kutoka kwa wakulima kutokana na vyama vingi vya msingi AMCO’S kuto tambua kwamba kiwanda hicho ni mali yao na hivyo wanapaswa kupeleka  kahawa kwa awingi katika kiwanda hicho badala ya kupeleka  viwanda vingine.


CHANG’A alisema kuwa  kwa vile kwa sasa kiwanda  hicho kinakabiliwa na ushindani mkubwa  amewataka AMCO’S  hizo kupeleka kahawa katika kiwanda chao ambacho wanahisa nacho ili kujiongezea kipato kwenye ushirika wao ikiwa ni Pamoja na kupata fursa mbali mbali ambazo zinatolewa kiwandani hapo kama vile  kuongeza nguvu wakati wa kuhudumia mashamba ya kahawa hiyo ikiwa mashambani ili kupata kahawa iliyo bora.


Amesema kuwa kiwanda hicho pia husaidia shughuli za maendeleo katika vijiji ambavyo AMCO’S zao zimepeleka kahawa katika kiwanda hicho kama vile kuchangia Saruji,Mabati kwenye ujenzi wa shule za Sekondari, shule za msingi na zahanati pamoja na majengo ya ofisi za vijiji au kata  kwa pale inapobidi.


Aidha amesema kuwa kiwanda hicho pia hutoa ajira kubwa kwa wakazi wa mbinga na walaya jiorani ambapo vijana wengi wa kiume na wa kike hupata ajira hiyo ya msimu na kujipatia kipata badala ya kuzurura na kwamba kama kahawa hiyo haipelekwi kwa wingi kiwandani hapo husababisha kuwepo kwa upungufu mkubwa wa ajira hasa  kwa akina mama na akina baba.


Hata hivyo amesema kuwa kwa msimu wa mwaka 2023/2024 kiwanda kimejipanga kikamilifu kuhakikisha kinapata kahawa kwa wingi kutoka katika AMCO’S na vikundi mbali mbali vinavyojishughulisha na  uzalishaji wa zao la kahawa na kukoboa kwa wakati kwa kadri ya mahitaji yao.


Kwa upande wake Afisa Masoko wa kiwanda hicho David Haule amesema kuwa kiwanda hicho  pia kinajishughulisha na usindikaji wa kahawa inayozalishwa mbinga ambayo inakuwa na ubora mkubwa na safi kwa matumizi ya kunywa na hivyo kukifanya kiwanda hicho kuendelea kuwa na ubora zaidi kutokana na kuhamasisha wakulima Pamoja na wananchi kwa ujumla kunywa kahawa inayolimwa na wenyewe.


Haule amesema kwamba baada ya kusindika kahawa hiyo nyingine husambazwa katika maeneo mbali mbali hapa Tanzania kama vile mikoa ya Dodoma, Dar es salaam, Tanga Lindi, Mtwara, Iringa na Mbeya ikwa ni Pamoja na maeneo mengine ambayo hayajatajwa na kwmba kahawa hiyo inapatikana kiwandani hapo kwa wale watakao hitaji kunywa kahawa yenye radha nzuri na ndiyo inayopendwa Duniani kote inapatikana muda  wote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post