HATUNA DENI NA MTATURU,AMELIPA NA CHENJI IMEBAKI




WAKAZI wa Kijiji cha Minyinga kilichopo Jimbo la Singida Mashariki Wilayani Ikungi Mkoani Singida,wamempongeza na kumshukuru Mbunge wa Jimbo hilo Miraji Mtaturu kwa kuwa daraja kati yao na serikali la kupeleka maendeleo na kusema mpaka sasa wana Minyinga hawana deni naye.

Akizungumza Juni 25,2023,katika mkutano wa hadhara wa Mbunge Mtaturu katika Kata ya Makiungu uliokuwa na lengo la kutoa mrejesho wa bajeti kwa wananchi na kusikiliza kero zao,Mwenyekiti wa Kijiji hicho Joshua Ikaku amesema Minyinga ya juzi sio sawa na ya leo.

“Minyinga ilikuwa imesahaulika,lakini leo tunajivunia uwepo wa Mtaturu,kuna siku niliwaambia hapa Minyinga hana deni amelipa yote,

“Kwa juhudi zake leo Minyinga tuna shule nzuri,kwa kweli tunafurahia maendeleo ambayo huko nyuma miaka iliyopita hatukuyaona ,ahsante sana mbunge wetu,umelipa deni na chenji imebaki,”amesema Mwenyekiti huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post