DC TANGA AZINDUA MSIMU WA SITA WA TANGA WOMEN GALA, AWAFUNDA WAJASIRIAMALI TANGA

 

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kushoto akizundua msimu wa sita wa Tanga Women Gala Jijini Tanga linaloandaliwa na Kampuni ya Five Brother Intertainment kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Nasoro Makau na kulia ni Mratibu wa Matukio Five Brothers  Asma Makau akifuatiwa na Naibu Meya wa Jiji la Tanga Wakili Mwanaidi Kombo
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kushoto akimvalisha kofia mmoja wa wajasiriamali waliofika kwenye uzinduzi huo 
Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tanaga Women Gala
Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Intertainment ambao ndio waandaaji wa Tanga Women Gala  Nasoro Makau akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Naibu Meya wa Jiji la Tanga (CCM) Wakili Mwanaidi Kombo akizungumza katika uzinduzi huo
Mwanzilishi wa Tanga Women Gala Latifa Shehoza akizungumza wakati wa uzinduzi huo 

Mwanzilishi wa Tanga Women Gala Latifa Shehoza  akiingia ukumbini wakati wa uzinduzi huo
Naibu Meya wa Jiji la Tanga Wakili Mwanaidi Kombo akiingia ukumbini 
Sehemu ya Wajasiriamali walioshiriki kwenye uzinduzi huo
Sehemu ya Wajasiriamali walioshiriki kwenye uzinduzi huo
Sehemu ya Wajasiriamali walioshiriki kwenye uzinduzi huo
Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kulia akiteta jambo na Naibu Meya wa Jiji la Tanga (CCM) Wakili Mwanaidi Kombo wakati wa uzinduzi huo

Na Mwandishi Wetu, TANGA


MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amezindua msimu wa sita wa Tanga Women Gala huku akitumia jukwaa hilo kuwataka wajasiriamali  watumie maonesho hayo kama sehemu ya kutangaza biashara zao na sio ya kufikiria ya kuuzia tu biashara .

Mgandilwa aliyasema hayo wakati akizungumza na wajasiriamali hao kwenye uzinduzi huo ambapo alisema kwamba miongoni mwao wakifika kwenye maonesho wanafikiria kuuza mzigo walionao kwa siku hizo wakimaliza wanasema faida wamepata mwisho wa siku wanaendelea na maisha.

Tanga Women Gala ni Jukwaa la Wajasiriamali ambalo limekuwa likifanyika kila mwaka kwa lengo la kuhakikisha wanakua na kuinuka kiuchumi kwa kupanua wigo wa kuwakutanisha linaloandaliwa na Kampuni ya Five Brother Intertainment

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wabadilike na kuondokana na hali hiyo badala yake watumie kama jukwaa la kutafuta masoko muda wote kwa kujikita kutangaza biashata zao na sio kuuza tu wakati wa maoyesho.

Alisema kwamba ni matumaini yake kwamba katika msimu huo wa sita wa Tanga Women Wajasiriamali tunakwenda kutengeneza historia kubwa ambayo itakuwa chachu ya kuendelea kuwainua wajasiriamali mkoani humo kukua kiuchumi

“Niwashukuru Tanga Women Gala kwa kazi kubwa mnaoendelea kuifanya tunajua inawezekana wakawa hawana cha kuwalipa lakini dua za wajasiriamali ambao kila siku mnaendelea kuwainua ndio malipo yenu”alisema Mkuu huyo wa wilaya.

“Pamoja na Pongezi mimi kama DC wenu niwapongeza kwa mchango wenu kwa jamii ya wana Tanga ni mkubwa serikali yetu imetengeneza fursa nyingi ikiwemo kutoa wigo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kufanya biashara zao vizuri bila changamoto zozote niliona kama kiongozi wa wilaya niwapongeza niwatake muendeee kufanya hivyo hivyo siku zote”Alisema

Hata hivyo aliwataka kuendelea kupanua wigo kwa wajasiriamali ambao kimsingi hawana uwezo wa kufika kwenye maeneo yao kwa kutengeneza utararibu wa namna ya kuweza kuwafikia na kuwatambua ili kuona namna ya kuwasaidia.

“Lakini maonyesho yetu ni ya siku chache ni vema tukajikita kutengeneza masoko baada ya maonyesho sio wakati wa maonyesho ninasema hivyo kwa sababu kwenye wakati huo tunakuwa na siku tatu mpaka tano hivyo tunapaswa kutegeneza kuona mjasiriamali anafanya biashara siku zote za mwaka”Alisema DC Mgandilwa,

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Five Bothers Intertainment Nasoro Makau alisema kwamba Tamasha hilo la Tanga Women Gala la msimu wa sita linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na namna walivyojipanga

Alisema kwamba wamekuja kuzindua rasmi siku pendwa uzinduzi huo ambao ni msimu wa sita mfululizo kwa umri wa kuzaliwa ni sawa na mtoto anayeanza shule Tanga huku akieleza Tanga Women Gala ilianza kwa hali ya udogo lakini sasa inakwenda kukua.

“Tunawashukuru wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya NMB,CRDB,Amana,Stanbic, Azania,TRA,Tanga Uwasana Prism Comunication ambao mwaka jana tuliokuwa nao hivyo tunaamini msimu huu pia watatushirika mkono tushirikiane nao”Alisema

Naye kwa upande wake Naibu Meya wa Jiji la Tanga (CCM) Wakili Mwanaidi Kombo alitoa wito kwa wakina mama kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo ili waweze kujikwamua kiuchumi

Mwanaidi ambaye pia ni Mrartibu wa Tawla Kanda ya kaskazini aliwataka pia kuona namna yao kufanya biashara kwa waledi ili ziwezi kuleta tija kwa maisha yetu na jamii zinazowazunguka.

“Wakati tukichangamkia fursa hizo tusisahau majukumu mengine kama mwanamke changamoto nyingi za ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanafunzi kwa sababu sisi wakinaa nana tumejikita kutafuta fedha badala ya majukumu yetu ya ndani”Alisema

Hata hivyo aliwataka wajiepushe na mikopo isiyokuwa na tija ya kausha damu riba zake hazieleki hivyo niwaombe kwamba iwapo wanataka kukua kiuchumi waende kwenye taasisi zilizosajiliwa za kifedha kwenye mabenki.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post