RC MNDEME AIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KUVUKA LENGO UKUSANYAJI MAPATO

 


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme ameipongeza Manispaa ya Shinyanga kwa kuvuka lengo ukusanyaji mapato

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (kuwapa maua yao), kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuvuka lengo, huku wakitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, pamoja na kupata Hati safi mara Tano mfulululizo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.

Mndeme amebainisha hayo leo Juni 24, 2023 kwenye kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga, cha kujadili Taarifa ya majibu ya Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha (2021/2022).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.

Amesema anawapongeza Manispaa ya Shinyanga kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani, ambapo mwaka wa fedha (2021/2022) walikusanya mapato asilimia 125, na mwaka wa fedha (2022/2023) hadi kufikia Juni 26 tayari wamesha kusanya mapato asilimia 102 na kuvuka lengo kabla hata ya kufika Juni 30 mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Baraza la Madiwani.

“Nawapongeza Manispaa ya Shinyanga kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato na mmekuwa mkitekeleza miradi mingi ya maendeleo kupitia fedha za mapato yenu ya ndani, na pia mmepata Hati safi mara tano mfululizo hivyo pokeeni maua yenu,”amesema Mndeme.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Arnold Makombe,akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani.

Aidha, akizungumzia Hoja za CAG amewataka Madiwani pamoja na Wataalamu washirikiane kwa pamoja kujibu hoja za CAG kwa kupeleka Viambatanisho au nyaraka muhimu za uhakiki ili kufuta hoja zilizosalia kujibiwa na kuendelea kupata Hati safi.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masubuko(kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Alexius Kagunze.

Naye Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Hesabu za Serikali (CAG) Patrick Malando, ameishauri Manispaa ya Shinyanga kuunda Timu Maalumu ambayo itakuwa ikihusika na uandaaji wa vitabu vya ukaguzi wa hesabu, ili ikitokea mmoja wapo hayupo basi pawepo na mtu mwingine, na kuondoa usumbufu wa kuanza upya kuandaa vitabu.
Naye Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Hesabu za Serikali (CAG) Patrick Malando.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amesema hoja zote zinajibika isipokuwa tatizo lililopo ni ukosefu wa nyaraka ya kwa ajili ya kuambatanisha kwenye ukaguzi, ambalo amedai linatokana na uzembe na kuahidi watazifuta hoja zilizosalia.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze, akisoma taarifa ya CAG amesema kwa kipindi cha kuishia Juni 30, 2022, Manispaa hiyo imepata Hati safi na ilikuwa na hoja 54 zilizoibuliwa na CAG, hoja 24 zimefungwa na kubaki 30 ambazo zinaendelea kutekelezwa kwa kuwasilisha majibu na Viambatanisho kwa Mkaguzi kwa ajili ya uhakiki.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze.
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao Maalumu cha Baraza cha kujadili hoja za CAG.
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao Maalumu cha Baraza cha kujadili hoja za CAG.
Diwani wa Kata ya Mjini Gulaam Hafeez akiwa kwenye kikao Maalumu cha Baraza cha kujadili hoja za CAG.
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao Maalumu cha Baraza cha kujadili hoja za CAG.
Diwani wa Masekelo Juma Nkwabi akiwa kwenye kikao Maalumu cha Baraza cha kujadili hoja za CAG.
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao Maalumu cha Baraza cha kujadili hoja za CAG.
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao Maalumu cha Baraza cha kujadili hoja za CAG.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, (kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi kwenye Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga la kujadili hoja za CAG.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo akiwa kwenye kikao maalum cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga cha kujadili hoja za CAG.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme wapili kutoka (kushoto) akipokewa na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye kikao maalumu cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga cha kujadili hoja za CAG.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post