PROF. MSHANDETE ASHAURI JESHI LA POLISI KUTUMIA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUBAINI WAHALIFU


Kaimu Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete akifungua kikao cha siku Moja ya utekelezaji wa makubaliano ya kujengeana uwezo na Jeshi la Polisi.
Kamishina wa Jeshi la Polisi kitengo cha Uchunguzi wa Kimtandao Bw Shabani Hiki akielezea umuhimu wa Sayansi na Teknolojia katika kubaini wahalifu.

Na Mwandishi Wetu 

Kaimu Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete ametoa wito kwa Jeshi la Polisi nchini kutumia Sayansi na Teknolojia kubaini wahalifu. 

Aliyasema hayo tarehe 21 Juni, 2023 wakati akifungua kikao cha kwanza cha utekelezaji wa mkataba wa makubaliano uliosainiwa baina ya taasisi hizo tarehe 31 Agosti ,2022 kwa lengo la kujengeana uwezo katika kutatua changamoto za kiuchunguzi kubaini wahalifu. 

 Profesa Mshandete alitoa wito kwa watumishi wa Jeshi la polisi nchini kupata ujuzi wa muda mfupi au mafunzo ya kisayansi na teknolojia kutoka katika taasisi hiyo yatakayowawezesha kuwabaini wahalifu. 

Kwa Upande wake Mkuu wa shule ya Sayansi ya Mawasiliano ya Komputa na Uhandisi Dkt Mussa Ali alisema, utekelezaji wa makubaliano ya kujengeana uwezo ,timu za utafiti kutoja shule ya Sayansi ya Mawasiliano ya Komputa na Uhandisi na Shule ya Biashara na Ubinadamu zinaifanyia kazi. 

Naye Kamishina wa Jeshi la polisi Bw. Shabani Hiki alieleza jinsi maabara za Jeshi la Polisi zinazofanya kazi zao za kiuchunguzi kwa kutumia ya sayansi na teknolojia.

 Aliongeza kuwa utumiaji wa Sayansi na teknolojia utasaidia upatikanaji wa matokeo chanya katika tafiti kuepuka kesi nyingi kurudishwa mahakamani kutokana ukosefu wa taarifa sahihi za mwalifu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post