MWANAMKE AJIFUNGUA KWENYE TRENI


Mwanamke mmoja nchini Kenya amejifungua wakati akiwa kwenye treni ya Madaraka Express iliyokuwa ikielekea Mombasa.

Kwa Mujibu wa mtandao wa Twitter wa shirika la reli la Kenya, mwanamke huyo alimkaribisha mtoto wake kwa usaidizi wa daktari ambaye alikuwa ndani ya usafiri huo na mhudumu wa abiria.

"Tulibarikiwa kuwa na Dkt. Indanyenyi Luseso ambaye alitoa huduma hiyo, akisaidiwa na Mhudumu wetu wa Abiria, Bi. Mary Nyiha" Shirika la Reli la Kenya liliandika pamoja na picha zinazoonyesha mhudumu akiwa amemshika mtoto.

Mwanamke huyo baadaye alikimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Mariakani kwa usaidizi zaidi wa kimatibabu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post