CHUO CHA UHASIBU ARUSHA CHAZINDUA DAWATI LA JINSIA

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka akizungumza na wadau wa Chuo hicho wakati wa uzinduzi wa Dawati la Jinsia uliofanyika tarehe 20 Juni 2023 chuoni hapo.
Baadhi ya Wafanyakazi, Wanafunzi na watoa huduma wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka (hayupo pichani), wakatii wa uzinduzi wa Dawati la Jinsia, uliofanyika tarehe 20 Juni 2023 chuoni hapo.
Mratibu wa Dawati la Jinsia Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA), Dkt. Theopil Assey akitoa taarifa kuhusu Dawati katika uzinduzi wa Dawati hilo uliofanyika tarehe 20 Juni 2023 chuoni hapo.
Mratibu wa Jinsia na Maendeleo ya Mtoto Jiji la Arusha, Bi. Habiba Madebe akiwasilisha Mada katika uzinduzi wa Dawati la Jinsia la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) uliofanyika tarehe 20 Juni 2023 chuoni hapo.
Mwakilishi Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi Arusha, Sagenti. Restituta akiwasilisha Mada katika uzinduzi wa Dawati la jinsia la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), uliofanyika tarehe 20 Juni 2023 chuoni hapo.
Baadhi ya Wafanyakazi, Wanafunzi na watoa huduma wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa Dawati la Jinsia, uliofanyika tarehe 20 Juni 2023 chuoni hapo.
Anyesi Mkolelwa ni mwanafunzi wa IAA akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake wakati wa uzinduzi wa Dawati la Jinsia, uliofanyika tarehe 20 Juni 2023 chuoni hapo.
Baadhi ya Wafanyakazi, Wanafunzi na watoa huduma wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa Dawati la Jinsia, uliofanyika tarehe 20 Juni 2023 chuoni hapo.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka (katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja Wajumbe wa Dawati la Jinsia la Chuo wakati wa uzinduzi wa Dawati la Jinsia, uliofanyika tarehe 20 Juni 2023 chuoni hapo.


Na Stella Kalinga, Chuo cha Uhasibu Arusha

Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) kimezindua rasmi Dawati la Jinsia likiwa na dhumuni kuelimisha Wanafunzi, Wafanyakazi pamoja na watoa huduma katika Chuo kuhusu umuhimu wa kuzingatia masuala ya kijinsia katika shughuli zao za kila siku.

Akizindua dawati hilo Juni 20,2023, Mkuu wa Chuo-IAA Prof. Eliamani Sedoyeka amesema dawati litawasaidia wadau hao kupata elimu juu ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia, hatua za kuzuia vitendo hivyo na namna ya kushughulikia endapo vitendo hivyo vitajitokeza.

“ Mtakapoona vitendo vyovyote vinavyoashiria unyanyasaji na ukatili wa kijinsia toeni taarifa kwa namna mtakavyoona inafaa ili mpatiwe msaada wa namna mbalimbali ikiwemo msaada wa kisaikolojia, msikae kimya,” amesema Prof. Sedoyeka.

Prof. Sedoyeka ameongeza kuwa uongozi wa Chuo utaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo, TAKUKURU, Dawati la jinsia la Polisi, Ofisi ya Mwendesha mashtaka wa serikali, pamoja na vyombo vingine katika suala la kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha IAA inakuwa sehemu salama.

Akiwasilisha mada Mratibu wa jinsia na maendeleo ya mtoto Jiji la Arusha Bi. Habiba Madebe amezitaja baadhi ya sababu zinazopelekea ukatili wa kijinsia katika jamii kuwa ni pamoja na mila, desturi, mmomonyoko wa maadili na mfumo dume, huku akisisitiza kuwa wako mstari wa mbele katika kupambana na ukatili huo.

Naye mwakilishi kutoka Dawati la jinsia la Polisi Arusha Sajenti Restituta ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limekuwa mstari wa mbele katika kupambana na ukatili wa kijinsia hasa mashuleni, vyuoni na katika jamii kwa ujumla na wamekuwa wakiwachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na ukatili huo.

Anyesi Mkolelwa ni mwanafunzi wa IAA aliyeshiriki katika uzinduzi huo, ameushukuru uongozi wa Chuo kwa kuanzisha dawati hilo, kwani utawasaidia wao kama wanafunzi kupata elimu na kuwa wa kwanza kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia hasa wakiwa Chuoni.

Uzinduzi huo umefanyika  IAA ukihudhuriwa na wanafunzi, wafanyakazi wa Chuo, watoa huduma, wawakilishi kutoa taasisi mbalimbali,pamoja wa wadau wengine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post