MAAFISA USHIRIKA KANDA YA MASHARIKI WAPEWA MAFUNZO KUIMARISHA USHIRIKA




Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Collins Nyakunga akifunga mafunzo ya usimamizi wa Ushirika kwa Maafisa Ushirika Kanda ya Mashariki, Mkoani Morogoro.

Na Mwandishi Wetu-MOROGORO

Maafisa Ushirika wametakiwa kutumia maarifa waliyopata kutokana na programu maalum ya mafunzo ya Usimamizi na Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika iliyoendeshwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa Maafisa Ushirika kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro.

Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Mrajis, Collins Nyakunga, wakati akifunga Mafunzo ya Maafisa Ushirika Mkoani Morogoro. Mafunzo ambayo yalizinduliwa Mei 17, 2023 na jumla ya Maafisa 72 wamehudhuria na kupata mafunzo ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika.

Naibu Mrajis amesema lengo la Tume kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa Maafisa Ushirika wanajengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao vyema ya kusimamia Vyama vya Ushirika ili viweze kujiendesha kwa tija na kupunguza changamoto na ambazo zimekuwepo katika Sekta ya Ushirika.

Sambamba na mafunzo hayo Maafisa Ushirika waliapishwa kutunza Siri mbele ya Hakimu Mkazi, Juma Ally Mbonde kwa lengo la kuhakikisha wanasimamia Vyama kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya utunzaji siri ili kuepusha uvujaji wa siri unaoweza kuleta madhara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments