WAZIRI NDALICHAKO ASHIRIKI KIKAO CHA MAWAZIRI KAZI NA AJIRA SADC




Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameshiriki Kikao cha Mawaziri wa Kazi na Ajira wa SADC kilichoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Gilbert F. Houngbo.

Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 29 Mei, 2023 kwa njia ya mtandao ambapo kupitia kikao hicho wameweza kujadili baadhi ya masuala yaliyojadiliwa na Bodi ya Magavana wa ILO mnamo mwezi Machi 2023 ambayo yatawasilishwa katika mkutano mkuu wa Shirika la Kazi Duniani utakaofanyika Juni 5 hadi 16, 2023 Geneva, Uswiss.

Masuala yaliyojadiliwa ni programu ya bajeti ya ILO kwa mwaka 2024/2025, hoja ya mabadiliko ya katiba ya ILO ili kuongeza demokrasia katika shirika hilo, ushirikishwaji wa wadau katika uendeshaji wa ILO kwa lengo ya kuongeza haki ya jamii na mapendekezo ya namna ya kuendesha vikao vya ILO vya kikanda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments