WAZIRI GWAJIMA AMUAGA ALIYEKUWA MUWAKILISHI MKAZI WA UNICEF BI.SHALINI BAHUGUNA JIJINI DODOMA
Na WMJJWM, Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameiongoza Menejimenti ya wizara hiyo kumuaga aliyekuwa muwakilishi Mkazi wa shirika la UNICEF nchini Tanzania Shalini Bahuguna katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma.

Waziri Dkt. Gwajima amemshukuru Shalini kwa ushirikiano aliyoipatia Wizara kwa kipindi cha mwaka 2020 mpaka 2023 alichokua akitimiza majukumu yake, hasa kwa kushiriki katika kuhakikisha ustawi na Maendeleo ya watoto Nchini.

Aidha, Waziri Dkt. Gwajima ametumia fursa hiyo kumkabidhi Bi. Shalini zawadi mbalimbali ikiwemo cheti cha kuthamini na kutambua mchango wake.

Kwa upande wake Bi. Shalin licha ya kuishukuru Wizara kwa ushirikiano, ameipongeza kwa utendaji, Ubunifu na uendeshaji wa weledi wa kwenye programu za mbalimbali katika kipindi chote walichokua wakishirikiana kuboresha hali za watoto nchini.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Wataalam kutoka Shirika la UNICEF Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post