JOSEPH KUSAGA ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO YA AJIRA NCHINI



Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Kampuni ya Clouds Media Group Joseph Kusaga ametunukiwa Tuzo ya Heshima ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake mkubwa ambao ameutoa katika kutatua changamoto ya ajira kwa Watanzania.

Tuzo hiyo ya Heshima imetolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Purple Planet ambayo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliamua kuandaa Jukwaa Maalum kwa kuwakutanisha wadau kujadili umuhimu wa kuendeleza sekta binafsi, kujitathimini baada ya janga la COVID-19 pamoja na utoaji tuzo.

Kwa mujibu wa waandaaji wa jukwaa hilo wameeleza kwamba kutolewa kwa tuzo hizo kwa wadau mbalimbali ambao wametoa mchango wao kwa jamii ya Watanzania unalenga kuwapa hamasa zaidi ya kuendelea kujitoa na kubwa zaidi ni kutambua watu wenye chachu na Mchango mkubwa kwenye sekta binafsi.

Pia sababu nyingine ya kutolewa kwa tuzo hizo ni kuamsha upya hari ya kufanya kazi ili kukuza uchumi wa watu binafsi na Taifa kwa ujumla.Hivyo taasisi hiyo kwa kutambua mchango wa Joseph Kusaga imeona ana kila sababu ya kupewa Tuzo ya Heshima kutambua mchango wake kwenye sekta binafsi kupitia kampuni yake ya Clouds Media Group ambayo imetatua changamoto ya ajira kwa kuajiri Watanzania.

Wengine waliopewa tuzo na taasisi hiyo ni Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Hajji Manara aliyepewa tuzo ya Watu wenye ushawishi na mchango kwenye ajira zisizorasmi na mitandao ya kijamii, Mwanamitindo maarufu nchini Speshoz Tanzania pamoja na Mama Tunu Pinda ambaye ni mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda.

Wakati wa Jukwaa hilo lililofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regence jijini Dar es Salaam wadau mbalimbali walihudhuriwa wakiwemo Wafanyakazi, Wafanyabiashara, na watu Mashuhuri walioalikwa katika usiku huo kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments