YANGA SC YANYAKUA UBINGWA 29 LIGI KUU TANZANIA BARAKLABU ya Yanga SC imeweka rekodi ikitwaa ubingwa wa 29 Ligi Kuu Tanzania bara Msimu wa 2022/23 baada ya kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Dodoma jiji mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex jijini la Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Kennedy Musonda dakika ya 39,Mudathir Yahya akifunga bao mawili dakika ya 70,90 na Farid Mussa dakika ya 88.

Mabao ya Dodoma jiji yamefungwa na Collins Opare dakika ya 59 na Seif Karihe dakika ya 67.

Ushindi huo unaifanya Yanga SC kutetea tena ubingwa wa Ligi Msimu huu ikiwa imefikisha Pointi 74 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote huku ikiwa imebakiwa na michezo miwili dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons itachezwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments