YANGA YATINGA NUSU FAINALI CAF


MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Yanga imewatoa kimasomaso watanzania baada ya kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kutoka sare ya kutofungana na Rivers United kutoka nchini Nigeria mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga imepata nafasi hiyo baada ya ushindi wa mabao 2-0 mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Nigeria.

Yanga ni kama inataka kufuata nyao za timu ya Simba ambayo Mwaka 1993 ilifanikiwa kutinga fainali za Kombe la CAF ikimenyana na Stella Abdijan Kutoka Ivory Coast ambapo hata hivyo haikufanikiwa kuchukua ubingwa

Simba SC ambayo ilikuwa inashikiriki Kombe la Klabu Bingwa Africa ilishindwa kutinga nusu Fainali ya klabu bingwa Afrika kwa kuondoshwa na Wydad Casablanca kwa mikwaju ya Penalti 4-3
Tanzania Sasa imeingiza timu moja nusu Fainali Katika michuano ya Kombe la Shirikisho ambalo zinacheza timu ambazo hazikufuzu Katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Hivi Sasa rasmi Yanga SC itakutana na Marumo Gallants kutoka Afrika Kusini waliwatoa Pyramids ya Misri kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mchezo wa kwanza wa nusu Fainali unatarajia kuchezwa Mei 14 au 15 mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kabla ya wiki moja marudiano kuchezwa nchini Afrika Kusini.

Timu nyingine ambayo zimefuzu Katika michuano ya Kombe la Shirikisho ni ASEC Mimosas ya Ivory Coastal baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir sasa inamsubiri Mshindi kati ya FAR Rabat ya Morocco au USM Alger ya Algeria ambao watacheza majira ya saa nne usiku.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments