BLOGA MAARUFU NCHINI UGANDA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI


Bloga mashuhuri kutoka taifa la Uganda Ibrahim Tusubira maarufu kama Isma Olaxess amepigwa risasi na kuuawa katika mtaa wa Kyanja katika jiji kuu la Kampala.

Olaxess ambaye alikuwa mwenyekiti wa muungano wa mabloga wa Uganda, alikuwa maarufu kwa video zake kwenye mitandao ya kijamii ambako aliwakosoa vikali wanasiasa. 

Bloga huyo hata hivyo pia alijishughulisha na masuala mengine kama vile video za kuburudisha na kufahamisha umma kuhusu masuala mbalimbali kama vile taarifa za watu mashuhuri. 

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Isma Olaxess alipigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana ambao walimwandama kutumia pikipiki akiwa njia kwenda nyumbani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post