AMUUA BABA YAKE KISHA KUMPIKA KAMA MBOGA


Mwanaume mmoja kutoka kijiji cha Giankaja, kaunti ya Tharaka Nithi alitiwa mbaroni baada ya kudaiwa kumuua baba yake na kupika sehemu za mwili wake.

Mwanamume huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi kaunti ya Tharaka Nithi nchini Kenya.

Polisi walithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha wakisema mwathiriwa ambaye ni mzee mwenye umri wa miaka 70, aliripotiwa kutoweka kwa siku tatu. Msako ulifanyika katika kijiji kizima na wakazi wa eneo hilo katika juhudi za kumtafuta mzee huyo.

Baada ya saa kadhaa za msako, upekuzi wao uliwaelekeza kwenye mtaro wenye kina kirefu ambapo waliupata mwili wa marehemu ambao tayari ulikuwa umeshaanza kuoza. 

Marehemu alikuwa amekatwa kichwa na sehemu za mwili wake kukatwa na miguu yake ikiwa kando ya mwili wake. Walikimbia haraka kwa chifu wa eneo hilo ili kumjulisha kuwa wamempata mtu aliyepotea. Hata hivyo, waliporejea kwenye mtaro, mwili huo haukuonekana.

Wakiwa wamechanganyikiwa na jinsi mambo yalivyobadilika, wenyeji hao katika udadisi wao pamoja na polisi na chifu walitafuta ndani zaidi ya mtaro. 

Walizunguka kwenye mtaro wa kina kirefu uliowaelekeza kwenye nyumba ambayo polisi wanasema huenda ilikuwa ya mshukiwa.

 Walipofika katika nyumba hiyo, walishangaa kupata chungu cha kupikia kimejaa nyama na mboga.

 Katika eneo la tukio, kulikuwa na fuvu la kichwa cha binadamu na nguo zilizojaa damu pamoja na viatu vya marehemu. 

Polisi walimhoji mshukiwa huyo kuhusu aliko baba yake lakini alibaini kuwa pia alikuwa hafahamu kwa kuwa anaendelea kumtafuta.

Sehemu nyingine za mwili zilizopotea ambazo ziligunduliwa kwanza na wenyeji zilipatikana zikiwa zimetupwa kwenye gunia na kufunikwa kwa mawe ndani ya Mto Nithi.

 Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambaye alidai kuwa mshukiwa huyo alianza kuchimba mtaro huo mwaka 2017, alieleza kuwa mshukiwa na mwathiriwa wake walizozana kuhusu hali ya mtaro huo kabla ya kupotea.

 "Wawili hao walizozana baada ya mwanaume huyo kumzuia babake kukata nyasi za Napier kuzunguka mtaro," Johnson Mutembei mkazi aliambia jarida moja la eneo hilo.

Kwa sasa mshukiwa yuko rumande akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

Chanzo- Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post