KIOTA KIPYA CHA KISASA KABISA 'FK LODGE' KIMEZINDULIWA MKOANI TABORA

Wafanyakazi wa FK Lodge wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkurugenzi wa FK Lodge , Bi Jane Matinde Kanga wakati wa Uzinduzi wa Lodge hiyo

****
Lodge mpya ijulikanayo kama FK lodge imezinduliwa mkoani Tabora na Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo. Lodge hiyo ya kisasa yenye vyumba 13 itaongeza upatikanaji wa malazi kwa wageni wa ndani na nje ya nchi wanaotembelea Mkoani hapo kwa sababu mbalimbali.

Akiongea wakati wa Uzinduzi Mkurugenzi Mkuu wa FK Lodge , Bwana Frederick Kanga amesema maono ya kuwekeza Tabora yameenda sambamba na kukuwa kwa haraka kwa mkoa Tabora hususani kwenye miundo mbinu ya Reli ya kisasa ambayo ikikamilika itaongeza mzunguko wa fedha na shughuli mbalimbali za kiuchumi kipindi cha ujenzi na hata baada ya reli kukamilika.


Uwepo wa barabara nzuri na za lami zinaziunganisha mikoa mingi ya jirani kama shinyanga , Singida, Mbeya, Kigoma, Katavi na Sumbawanga pia kutafanya Tabora kuwa kitovu cha biashara lakini pia kumekuwa na uhaba wa sehemu za malazi zinazoshabihiana na kasi hii ya ukuaji na maendeleo na hivyo tumeona ni vyema kuwekeza kwenye lodge ili kwenda sambamba na mahitaji haya muhimu.


Aidha uwekezaji huu utawezesha kuwepo kwa ajira kwa wakazi wa Tabora na Mikoa ya Jirani na hivyo kuchangia katika kukua kwa uchumi wa mkoa huu na nchi kwa ujumla

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Mh Molo Juma Molo Awapongeza sana wakurugenzi na wamiliki wa FK Lodge kwa kuwekeza Tabora na kuahidi kutoa ushirikiano katika kukuza na kuwepo kwa mazingira bora ya uendeshaji wa biashara na kutoa wito kwa wadau wengine hususani wawekezaji wa ndani kuwekeza katika Mkoa wa Tabora.

Akiongea huduma zinazopatikana Makamu Mkurugenzi wa FK Lodge , Bi Jane Matinde Kanga amesema lodge hii ina vyumba 13 vyenye huduma zote muhimu ikiwemo WiFi , lakini huduma za vyakula na vinywaji pia vinapatika katika lodge hii. Aliongeza kwa kusema”Tunajisikia fahari kuweza kutengeneza Ajira kwa vijana 9 zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi , kadhalika tumeingia mikataba makapuni mbalimbali ya kutoa huduma kama za broadband, ulinzi, maji , umeme na hivyo kuchangia katika ungezeko la mapato yao na hivyo kukuza uchumi na pato la taifa kupita kodi. Matumaini na maono yetu kuwa kuwepo kwa lodge hii ni mwanzo wa nyingine nyingi katika maeneo mbalimbali nchini”.

Kupata taarifa zaidi tembelea tovuti ya FK Lodge :
Mkurugenzi Mkuu wa FK Lodge , Bwana Frederick Kanga akiongea wakati wa uzinduzi wa FK lodge iliyopo Ipuli Tabora
Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo na Mkurugenzi Mkuu wa FK Lodge , Bwana Frederick Kanga wakikata keki wakati wa uzinduzi wa FK Lodge Tabora

Wamiliki wa FK Lodge Bwana na Bibi Frederick Kanga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa lodge mkoani Tabora
Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo akiangalia muonekano wa lodge ndani wakati wa uzinduzi wa lodge hiyo
Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo akiangalia muonekano wa lodge ndani wakati wa uzinduzi wa lodge hiyo
Wadau wa FK Lodge Joe na Mikidadi wakifungua champaign wakati wa uzinduzi
Wageni waalikwa wakipata chakula cha pamoja wakati wa uzinduzi
Baadhi ya wafanyakazi wa Exim walihudhuria uzinduzi wa FK Lodge mkoani Tabora

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post