SEKTA YA MAWASILIANO IMEKUWA NA MAENDELEO MAKUBWA YA KIUCHUMI NCHINI-MOHAMED

Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Khalid Salum Mohamed akizingumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika Tehama yaliyofanyika mjino Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Dkt.Jabir Bakari akitoa maelezo kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika Tehama yaliyofanyika Mjini Zanzibar.
Washindi wa Kwanza wakipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Khalid Salim Mohamed kwenye maadhimisho ya Wasichana katika Tehema , Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Washirika katika maadhimisho ya Wasichana katika Tehama, Mjini Zanzibar.

Baadhi ya Wanafunzi wa Wasichana katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa katika Tehama yaliyofanyika Mjini Zanzibar
*Dkt.Jabir aahidi kuendelea katika kuhakikisha wasichana wanakuwa wabunifu katika Tehama

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Serikali Mapinduzi Zanzibar Khalid Salum Mohamed miaka ya hivi karibuni kumekuwa na maendeleo makubwa katika sekta ya mawasiliano hapa nchini. Jamii kubwa ya watanzania mijini na vijijini imefikiwa na huduma za mawasiliano ya simu na mtandao wa intaneti.

Waziri Mohamed ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika Tehama yaliyofanyika mjini Zanzibar.

Amesema TCRA imeshiriki kikamilifu katika kufanya utafiti kwa ajili ya ujenzi wa minara 45 ya Mawasiliano ya simu kwenye maeneo mbalimbali hapa Zanzibar ambayo yalikuwa yakipokea huduma hafifu za Mawasiliano na baadhi ya maeneo hayakuwa na huduma kabisa na minara yote inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

"Nimearifiwa pia kuwa, hadi mwezi Machi 2023, idadi ya watumiaji wa intaneti imeongezeka hadi kufikia watu milioni 33, na idadi ya watumiaji laini za simu kufika milioni 61. Hii inaonesha kwamba Tanzania ni nchi ambayo watu wake wanaweza kupata huduma mbalimbali za mawasiliano kwa gharama nafuu ikilinganishwa na nchi nyingine duniani na kuongeza

upatikanaji na unafuu wa huduma mbalimbali za mawasiliano nchini ni uthibitisho tosha kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimejipanga vilivyo kuandaa mazingira bora na wezeshi kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa kidijitali" amesema Mohamed

Amesema mazingira ya uboreshaji wa mawasiliano yamesaidia utoaji wa huduma za kijamii, kufikia watu wengi zaidi katika maeneo ya mijini na vijijini, kuzalisha ajira, kuongeza pato la taifa, kufungua fursa mpya za maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii nchini na hivyo kuboresha maisha ya wananchi" amesema Mohamed

Amesema Serikali ya Tanzania na SMZ zimekuwa zikifanya jitihada kubwa kuhakikisha wananchi wake wanapata ujuzi wa kutumia teknolojia za kidigitali kwa lengo la kuwaendeleza kiuchumi, kielimu na kijamii. Mitaala ya vyuo vikuu, shule za sekondari na msingi imeboreshwa kuwezesha ufundishaji wa masomo ya TEHAMA yanayokwenda na kasi ya mabadiliko ya teknolojia na kumwezesha mwanafunzi kutumia teknolojia hizo kufanya ubunifu wa kutatua changamoto za kijamii.

Amesema TCRA kwa jitihada zao katika kuelimisha jamii, hususani vijana na kipekee wasichana na wanawake kuwawezesha kupenda na kujifunza masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi, na hisabati kutokana umuhimu wa hayo masomo

Amesema wasichana wanahitaji kuungwa mkono katika kujifunza masomo ikiwa TCRA kwa kuwezesha na kuhamasisha wasichana katika kufikia ndoto zao.

Mohamed amesema TCRA imeanzisha vilabu vya kidigitali katika vyuo na shule kwa lengo la kukuza ujuzi wa kigiditali (digital skills) na kuwezesha vijana kupata elimu bora juu ya matumizi salama ya teknolojia za kidigitali. Hatua hii inalenga kuwasaidia vijana kujenga ujuzi wao wa kiteknolojia na hatimaye kuchangia katika maendeleo ya jamii zao kwa kufanya ubunifu mbalimbali.

Aidha amesema TCRA imeanzisha vilabu hivi hapa Zanzibar vilivyopo Unguja na Pemba kwani ni hatua kubwa na muhimu katika kuendeleza TEHAMA na kukuza ujuzi wa TEHAMA kwa vijana.

Pia amepongeza kufanyika kwa mafunzo kwa ajili ya wasichana yamefanyika kwa mafanikio hapa Zanzibar. Nimeelezwa kuwa jumla ya wasichana 80 wamepata mafunzo haya; 30 katika kituo cha Unguja na 50 katika vituo viwili vya Pemba. Hii ni hatua muhimu katika kuwawezesha wasichana na kuwapa nafasi sawa na wavulana katika ujifunzaji wa TEHAMA.

Amewataka wakuu wa vyuo na shule za Sekondari hapa Zanzibar kuhakikisha kuwa kila chuo na Skuli ya Sekondari inakuwa na Klabu ya Kidijitali ili kuwahamasisha vijana wetu kupata ujuzi wa TEHAMA, ambao utasaidia kuleta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii. Ujuzi huu ni muhimu sana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili jamii yetu. Kama mnavyoona katika mawasilisho yaliyotolewa hapa, teknolojia ina jukumu muhimu katika kuboresha maisha yetu. Kwa hiyo, ni muhimu sana kwa shule na vyuo kutoa fursa hizi kwa wanafunzi wao ili waweze kuwa na ujuzi wa kutosha wa TEHAMA na kuchangia katika kuleta maendeleo ya jamii yetu.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Bakari amesema Siku ya Wasichana na TEHAMA Duniani, huadhimishwa kila mwaka imetokana na makubaliano ya nchi wanachama wa Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU), ambapo TCRA ni mwakilishi wa Tanzania katika shirika hilo.

Amesema kuwa TCRA kwa kushirikiana na wadau wa elimu yaani (TAMISEMI, Wizara ya Elimu, TCU na NACTVET) kwa sasa wanaandaa Mwongozo utakaoelezea bayana namna ya kuanzisha na kuendeleza klabu za kidijitali katika shule za msingi, sekondari na vyuo.

TCRA inaamini kuwa kupitia klabu za Kidijitali katika kuongeza wabunifu wenye umri mdogo, wataalamu katika sekta ya Mawasiliano, ambayo ni sekta wezeshi

Kutoa elimu endelevu kwa wadau waliopo katika shule Kurahisisha mawasiliano pale panapokuwa na pengo la uelewa Dkt.Bakari klabu za wanafunzi zinatumika kwenye kufikisha ujumbe wa kuhakiki laini za simu Kuwezesha wahusika kupata uelewa wa sekta ndogo tatu za mawasiliano.

Amesema wanathamini mchango sekta ya Mawasiliano katika maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii kuona wasichana katika Taifa letu wanapata fursa ya kujifunza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kupata wataalamu watakaolisaidia Taifa kupiga hatua zaidi katika maendeleo hasa ukuzaji wa uchumi wa Kidijiti na uchumi wa buluu.

Dkt.Jabiri amesma kuwa Kauli mbiu ya siku ya Wasichana na TEHAMA duniani kwa mwaka huu inasema “Ujuzi wa Kidijiti kwa Maisha”lengo la kauli mbiu hii ni kuhamasisha mafunzo na ujuzi wa Kidijiti kwa wasichana na wanawake ili kuongeza ubunifu katika sekta ya TEHAMA kama tunavyofahamu kuwa msingi wa maendeleo katika jambo lolote ni kupata mafunzo sahihi na kutumia taaluma hiyo kwa manufaa yako binafsi na jamii kwa ujumla.

Aidha amesema TCRA huadhimisha siku hii kila mwaka kwa kuandaa matukio mbalimbali ambayo ni semina, midahalo kwa wasichana wa shule nchini kuhusu masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na TEHAMA kwa ujumla.

Amesema TCRA iligawa vifaa vya TEHAMA (kompyuta) kwa shule 15 za wasichana Tanzania bara na visiwani, kwa lengo la kuhamasisha wasichana kujifunza masomo ya TEHAMA ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za ukuaji wa sekta. Aidha, kila mwaka, Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) hutoa kauli mbiu maalum inayohusu TEHAMA na mchango wake katika maendeleo ya jamii kwa ajili ya kuadhimisha maadhimisho hayo.

Amesema kwa kuzingatia Kauli Mbiu ya mwaka huu, "Ujuzi wa Kidijiti kwa Maisha", ni muhimu kuelewa kwamba ujuzi huu unaweza kuwa na athari chanya katika maisha yetu, hata kama unaanza kupata ujuzi huu kwa kiwango kidogo.

Amesema TCRA imeratibu mafunzo ya muda mfupi ya TEHAMA kwa wanafunzi wasichana wa vyuo vikuu kupitia vilabu vya Kidijiti vilivyopo katika Mikoa ya Unguja na Pemba, Morogoro, Dodoma, Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, na Mwanza.

Mafunzo haya yanajenga uwezo, ubunifu na ujuzi kwa wasichana katika kuandaa Programu Tumizi zitakazotatua changamoto katika jamii, pamoja na kuwapa fursa ya kujifunza ubunifu zaidi. Katika kipindi cha mafunzo ya siku nne, wanafunzi walipewa jukumu la kutambua tatizo la kijamii, kulichambua, na kupanga jinsi ya kutumia TEHAMA kutatua changamoto husika.

Hata hivyo amesema mafunzo yalijumuisha kutengeneza muundo wa mfumo kuandaa namna ya kuutekeleza kwa njia ya mtandao kwa kutumia simu kutengeneza programu ya rununu), na hatimaye kuandaa mfumo wenyewe.

Amesema Wanafunzi waligawanywa katika vikundi tisa na walishindanishwa kulingana na ufanisi wa mipango yao na kuweka vigezo vya mchujo viliandaliwa, na siku ya mwisho ya mafunzo, wanafunzi walipata fursa ya kuwasilisha na kuelezea kazi zao kwa waratibu na walimu wa programu hii. Kikundi kimoja kilichofanya vizuri zaidi kilitambuliwa kupitia vigezo vya mchujo na kushindanishwa na washindi kutoka vilabu vingine nchini. Hatimaye, vikundi vitatu vilivyofanya vizuri zaidi vilichaguliwa.

"Tunatambua na kuthamini mchango wenu katika kufanikisha kazi hii, tunawaasa muendelee kuwaendeleza vijana hasa wasichana, kwa kuwajengea uwezo kwenye masomo ya STEM kwa ujumla na kwa upande wa TEHAMA muendelee kusisitiza matumizi salama ya TEHAMA " Amesema Dkt.Bakari

Amesema wanatarajia kwamba mtakuwa chachu kuwahamasisha wenzenu kupenda masomo ya Sayansi ili kuongeza ujuzi wa Kidijiti na pia kujiunga na vilabu vya Kidijiti katika vyuo na shule zenu.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Bakari amesema Siku ya Wasichana na TEHAMA Duniani, huadhimishwa kila mwaka imetokana na makubaliano ya nchi wanachama wa Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU), ambapo TCRA ni mwakilishi wa Tanzania katika shirika hilo.

Amesema kuwa TCRA kwa kushirikiana na wadau wa elimu yaani (TAMISEMI, Wizara ya Elimu, TCU na NACTVET) kwa sasa wanaandaa Mwongozo utakaoelezea bayana namna ya kuanzisha na kuendeleza klabu za kidijitali katika shule za msingi, sekondari na vyuo.

TCRA inaamini kuwa kupitia klabu za Kidijitali katika kuongeza wabunifu wenye umri mdogo, wataalamu katika sekta ya Mawasiliano, ambayo ni sekta wezeshi Kutoa elimu endelevu kwa wadau waliopo katika shule Kurahisisha mawasiliano pale panapokuwa na pengo la uelewa.

Amesema klabu za wanafunzi zinatumika kwenye kufikisha ujumbe wa kuhakiki laini za simu Kuwezesha wahusika kupata uelewa wa sekta ndogo tatu za mawasiliano.

Amesema maadhimisho hayo ni kuwahamasisha wasichana kuchukua masomo ya Sayansi (STEM) ambayo ni Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati na kuwaonesha fursa zilizopo katika sekta wa TEHAMA ambazo wao kama wasichana wanaweza kunufaika nazo iwapo wataweka bidii.

Amesema wanathamini mchango sekta ya Mawasiliano katika maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii kuona wasichana katika Taifa letu wanapata fursa ya kujifunza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kupata wataalamu watakaolisaidia Taifa kupiga hatua zaidi katika maendeleo hasa ukuzaji wa uchumi wa Kidijiti na uchumi wa buluu.

Dkt.Jabiri amesma kuwa Kauli mbiu ya siku ya Wasichana na TEHAMA duniani kwa mwaka huu inasema “Ujuzi wa Kidijiti kwa Maisha”lengo la kauli mbiu hii ni kuhamasisha mafunzo na ujuzi wa Kidijiti kwa wasichana na wanawake ili kuongeza ubunifu katika sekta ya TEHAMA kama tunavyofahamu kuwa msingi wa maendeleo katika jambo lolote ni kupata mafunzo sahihi na kutumia taaluma hiyo kwa manufaa yako binafsi na jamii kwa ujumla.

Aidha amesema TCRA huadhimisha kila mwaka kwa kuandaa matukio mbalimbali ambayo ni vsemina, midahalo kwa wasichana wa shule nchini kuhusu masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na TEHAMA kwa ujumla.

Amesema TCRA iligawa vifaa vya TEHAMA (kompyuta) kwa shule 15 za wasichana Tanzania bara na visiwani, kwa lengo la kuhamasisha wasichana kujifunza masomo ya TEHAMA ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za ukuaji wa sekta. Aidha, kila mwaka, Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) hutoa kauli mbiu maalum inayohusu TEHAMA na mchango wake katika maendeleo ya jamii kwa ajili ya kuadhimisha maadhimisho hayo.

Amesema TCRA imeratibu mafunzo ya muda mfupi ya TEHAMA kwa wanafunzi wasichana wa vyuo vikuu kupitia vilabu vya Kidijiti vilivyopo katika Mikoa ya Unguja na Pemba, Morogoro, Dodoma, Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, na Mwanza.

Mafunzo haya yanajenga uwezo, ubunifu na ujuzi kwa wasichana katika kuandaa Programu Tumizi zitakazotatua changamoto katika jamii, pamoja na kuwapa fursa ya kujifunza ubunifu zaidi. Katika kipindi cha mafunzo ya siku nne, wanafunzi walipewa jukumu la kutambua tatizo la kijamii, kulichambua, na kupanga jinsi ya kutumia TEHAMA kutatua changamoto husika.

Amesema Wanafunzi waligawanywa katika vikundi tisa na walishindanishwa kulingana na ufanisi wa mipango yao na kuweka vigezo vya mchujo viliandaliwa, na siku ya mwisho ya mafunzo, wanafunzi walipata fursa ya kuwasilisha na kuelezea kazi zao kwa waratibu na walimu wa programu hii. Kikundi kimoja kilichofanya vizuri zaidi kilitambuliwa kupitia vigezo vya mchujo na kushindanishwa na washindi kutoka vilabu vingine nchini. Hatimaye, vikundi vitatu vilivyofanya vizuri zaidi vilichaguliwa.

"Tunatambua na kuthamini mchango wenu katika kufanikisha kazi hii, tunawaasa muendelee kuwaendeleza vijana hasa wasichana, kwa kuwajengea uwezo kwenye masomo ya STEM kwa ujumla na kwa upande wa TEHAMA muendelee kusisitiza matumizi salama ya TEHAMA " Amesema Dkt.Bakari

Amesema wanatarajia kwamba mtakuwa chachu kuwahamasisha wenzenu kupenda masomo ya Sayansi ili kuongeza ujuzi wa Kidijiti na pia kujiunga na vilabu vya Kidijiti katika vyuo na shule zenu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments