HYATT REGENCY WARUDISHA SHUKRAN KWA JAMII WACHANGIA DAMU.

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WATUMISHI wa Hoteli za Hyatt Regency warudisha shukrani kwa  jamii kwa kuchangia damu katika kuokoa maisha ya watu  wenye uhitaji katika hospitali mbalimbali zilizopo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo  Aprili 24, 2023 Jijini Dar es Salaam Meneja  Mkuu wa Hoteli ya Hyatt Regency Alexander Eversberg amesema suala la  kurudisha kwa jamii ni kutokana na huduma wanazotoa wameamua kufanya hivyo kwa kuchangia damu salama  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wateja wao pamoja  na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.

Amesema kila ifikapo mwezi Aprili kila  mwaka,  Hoteli zote za Hyatt Regency hurudisha kwa jamii kwa  kufanya shughuli mbalimbali ambazo  zinagusa moja kwa moja jamii  ikiwemo kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya mji,kutoa msaada kwa vituo vya watoto yatima au kuchangia damu.

Nae Afisa wa Rasilimali Watu Hoteli ya Hyatt Regency Bi.Iddah Mushi amesema kwa kuwa wamekuwa wakiwasiliana na watu wa benki ya damu salama,  wameona kumekuwa na uhaba mkubwa wa damu na uchangiaji ni mdogo kwa hiyo wameona kushirikiana na wadau wengine ili kufanya zoezi hilo ili kugusa jamii mmoja mmoja

Kwa upande wake Afisa Uhamasishaji Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki Bi.Mary Meshi ameipongeza Hyatt Regency kwa kutambua kutoa damu ni sehemu ya maisha ya kila mmoja na kuamua kutoa sehemu ya kurudishia katika jamii.

"Tumekuwa na uhitaji mkubwa wa damu hivi karibuni kutokana na waau muhimu wa uchangiaji damu  kuwa katika shughulli za mfungo kwahiyo Hyatt kujitokeza na kuweza kusaidia hili katika ukusanyaji wa damu kwetu sisi ni faida". Amesema 

Aidha ametoa wito kwa maofisi na Taasisi zingine kuendelea kuchangia damu ili kuweza kuokoa  maisha ya watu wengine kwani hatuwezi  kupata damu salama bila jamii kujitoa kwa moyo kuchangia damu.

Comfort Fidel ambaye ni Mwanafunzi wa IFM amesema wameamua kuungana na wadau katika kushiriki uchangiaji wa damu salama kwasababu kumekuwa na changamoto ya damu nchini hivyo wakaona kuna umuhimu  mkubwa wa kushiriki zoezi hilo na kuweza kuhamasisha vijana wengine kuona jambo hilo ni la muhimu katika kusaidia jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Hyatt Regency Alexander Eversberg akichangia damu leo Aprili 24,2023 katika zoezi hilo ambalo liliwakutanisha watumishi wa Hyatt Regency pamoja na wadau mbalimbali katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam


Mmoja wa wadau ambao wamejitokeza leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam na kuchangia damu Salama leo Aprili 24,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Hyatt Regency Alexander Eversberg akifanyiwa vipimo kabla ya kuchangia damu leo Aprili 24,2023 katika zoezi ambalo liliwakutanisha watumishi wa Hyatt Regency pamoja na wadau mbalimbali katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam
Wataalam mbalimbali kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama wakitoa maelezo kwa wadau mbalimbali waliojitokeza katika zoezi la uchangiaji damu leo Aprili 24,2023 katika Hoteli ya Hyatt regency Jijini Dar es Salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments