UJENZI WA BARABARA YA MIKUMI - IFAKARA WAFIKIA 78%, MIRADI MINGINE MITANO KUJENGWA MOROGORO

Wakati ujenzi wa barabara ya Mikumi hadi Ifakara kwa kiwango cha Lami ukifikia asilimia 78, miradi mingine mitano ya barabara inatarajiwa kujengwa mkoani Morogoro.


Akizungumza na waandishi, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoa wa Morogoro, Alinanuswe Kyamba amesema ujenzi wa barabara hiyo unaohusisha pia ujenzi daraja la Ruaha Mkuu unatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.


"Hadi kufikia Aprili 2023, utekelezaji wa mradi kwa ujumla ulikuwa umefikia asilimia 78, kwa sasa Mkandarasi amekamilisha km 43 za lami na kazi zingine zinaendelea kwa hatua nzuri. Madaraja yote yameshakamilika kwa asilimia 83 na daraja la Ruaha mkuu bado kitako cha juu kukamilika," amesema.


Amesema kukamilika kwa daraja la Ruaha Mkuu kutafanya magari mawili kupita kwa wakati mmoja tofauti zamani.


Amesema wa mradi huo ulianza mwaka 2018 lakini changamoto mbalimbali ikiwemo mvua umetajwa kuwa sababu ya kuchelewa kukamilika kwa mradi huo.


"Pia Mlipuko wa homa ya Mapafu (COVID -19) ilichangia kuwapo kwa ucheleweshwaji wa uangizaji wabaadhi ya vitendea kazi kwa ajili ya mradi.

Mbali na barabara hiyo pia mkoa wa Morogoro unakwenda kutekeleza miradi mingine mitano ambayo itakwenda kuunganisha wilaya zote kwa kiwango cha lami na kuinua uchumiwa Wananchi wa maeneo hayo.


Kwa mujibu wa Kyanda miradi yote imekwishatangazwa zabuni na iko katika hatua za mwisho ili kuweza kusaini mikataba


Miradi hiyo ni ule wa barabara ya Ubena Zomozi – Ngerengere (Kizuka Army Camp) yenye urefu wa 11.6km, Mradi wa ujenzi wa barabara ya Ifakara – Kihansi – Mlimba – Taweta – Madeke, Sehemu ya Ifakara – Mbingu, km 62.5.


"Pia kuna Mradi wa ujenzi wa barabara ya Ifakara – Kihansi – Mlimba – Taweta – Madeke, Sehemu ya Mbingu – Chita JKT, yenye urefu wa Km 37.5.


Mradi mwingine alioutaja ni ule wa wa barabara ya Bigwa – Kisaki (sehemu ya Bigwa –Mvuha, km 78, Pamoja na Madaraja ya Ruvu na Mvuha.


"Mradi wa mwisho utakuwa ni wa ujenzi wa barabara ya Ifakara – Lupiro – Mahenge / Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Lumecha na Malinyi JCT – Malinyi, km 422.54.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post