TASAF: USHIRIKISHWAJI WA KUNUSURU KAYA ZA WALENGWA UTAHUSISHA NCHI NZIMA BARA NA VISIWANI



Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Ladislaus Mwamanga akizungumza katika Kikao kazi cha wadau kwa ajili ya kupokea maoni kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa uliofanyika kwenye ofisi za TASAF jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Aprili 13,2023.

..................................................

Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Ladislaus Mwamanga amesema lengo kubwa la TASAF ni kuhakikisha ushirikishwaji kaya za watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa unahusisha nchi nzima Tanzania Bara na Zanzibar ili kukwamua kaya hizo katika lindi laumasikini

Akizungumza kwenye Kikao kazi cha wadau kwa ajili ya kupokea maoni kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa amesema lengola kikao hicho ni kupokea maoni kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa.

"Serikali kupitia mpango huu imeamua kutoa ruzuku Maalumu kwa kaya za watu wenye ulemavu Ili kuwaongezea uwezo wa kufanya majukumu yao,". Amesema Ladslaus Mwamanga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Suzana Mayengo amsema ujumuishaji na uimarishaji kwa watu wenye ulemavu utaliwezesha kundi hilo kupata maendeleo na kuondokana na umasikini

Ameutaka mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kuhakikisha inajumuisha na kuimarisha kaya za watu wenye ulemavu Ili kuwezesha kundi hilo kupata maendeleo

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan Iko mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wake wanaondokana na umasikini sambamba na kushiriki Shughuli mbalimbali za maendeleo

Naye Mwenyekiti wa Shirikusho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania Ernest Kimaya ameshukuru serikali kwa kushirikisha watu wenye ulemavu kwenye mpango huu ambapo kwa sasa kundi hilo limekuwa likiweza kutoa mchango kwa familia zao

Hata hivyo ameionba serikali kuangalia namna ya kusaidia kundi la watu wenye ulemavu kwenye nafasi za ajira pindi fursa zinapopatikana



Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Ladislaus Mwamanga akizungmza katika Kikao kazi Cha wadau kwa ajili ya kupokea maoni kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa uliofanyika kwenye ofisi za TASAF jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Aprili 13,2023, kulia ni Ernest Kimaya Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) na kushoto ni Ussy Khamis Debe Ktibu Mtendaji Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar. Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Suzana Mayengo akizungumza katika kikao hicho.

Meneja Rasirimali Watu wa TASAF Bi. Mariam Al Jabir kushoto na Zuhura Mdungi Mtaalam wa Mawasiliano TASAF wakifuatilia mawasilisho ya kikao kazi hicho.


Picha zikionesha washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini wakishiriki katika kikao kai hicho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post