CHUO CHA MZUMBE KUZITAFUTIA MASOKO BUNIFU ZINAZOIBULIWA NA WANAFUNZI WAKEKaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la chuo hicho katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha,akizungumza na watumishi wa chuo hicho katika banda la chuo hicho katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa chuo hicho wakati wa kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

CHUO Kikuu cha Mzumbe kimesema kitaendelea kuibua,kuendeleza na kuzitafutia masoko bunifu mbalimbali zinazoibuliwa na wanafunzi wa chuo hicho huku kikidai tayari ina kitengo maalum kwa kusimamia bunifu hizo.

Hayo yameelezwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha wakati akizungumza katika banda la chuo hicho katika maonesho ya wiki ya ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Prof Mwegoha amesema wanayafurahia maonesho hayo kwani yanahamasisha bunifu mbalimbali pamoja na masuala ya Sayansi na Teknolojia.

Amesema Mzumbe wanachokifanya ni kuhakikisha wanapromoti bunifu mbalimbali za wanafunzi wao ambapo amedai kwa sasa wana Kitivo cha Sayansi na Teknolojia.

Amesema katika mambo wanayofanya katika kitivo hicho ni pamoja na wanafunzi kuja na bunifu mbalimbali ambazo zinaenda kutatua changamoto za wananchi.

Amesema bunifu ambazo wamekuja nazo ni kwa ajili ya kupambana na changamoto za afya,mazingira,usafirishaji na uchukuzi.

“Sasa hivi tuna kitengo maalum kabisa kwa ajili ya kusimamia bunifu,baada ya hapa hawa vijana ili zile waweze kuzitangaza zifike mahali ambako wataweza kutengeneza biashara ambazo zitawainua kiuchumi.

“Hii inaendana na sera ya kitaifa ya kuhakikisha kwamba vijana wanajiajiri vijana wanaokuja hapa wanakuja na mawazo yao na tunawapa ushuri na baadae kuzigeuza kuwa biashara ikiwa ni pamoja na kuwatafutia wafanadhili ambao watazikuza,”amesema Prof Mwegoha

Amesema kupitia kituo hicho cha ubunifu wameanza kwenye kituo atamizi ambacho kinawataalamu kwa ajili ya kukuza idea zao.

Amesema chuo kinakiwezesha kitengo hicho ili kuendeleza miradi na waendelee kuwepo na kuwafikisha katika ndoto zao.

“Tutaendelea kuzisapoti mpaka pale ambapo wanaweza kuziendeleza na kuwa fursa.Hata wakiamua kwenda kufanya hizo kazi wana mahali pa kuanzia,”amesema Prof Mwegoha

Amesema katika bunifu walizokuja nazo ni pamoja na jiko ambalo linatumia mkaa wa taka kwa ajili ya kulinda mazingira.

“Katika bunifu ambazo tumekuja nazo ni jiko ambalo linatumia mkaa wa taka kwa ajili ya nishati na hii ni moja ya bunifu ambazo zipo nyingi ili serikali ikipiga marufuku mkaa tuweze kusapoti, majiko yanatumia taka lakini yanatoa nishati kubwa,”amesema Prof Mwegoha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post