Shuhudia Hapa : MAZISHI YA MFANYABIASHARA MAARUFU MUSOMA FOOD

Mazishi ya mwili wa Mfanyabiashara wa nafaka mkoa wa Shinyanga/Mkurugenzi wa Kampuni ya Musoma Food, Boniphace Said Makilagi maarufu Musoma Food yamefanyika leo Alhamisi Aprili 6,2023 nyumbani kwake Kambarage Mjini Shinyanga.

Mazishi ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Musoma Food yamehudhuriwa na maelfu ya waombolezaji kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.


Kwa mujibu wa taarifa ya familia tarehe 27.5.2021 Said Makilagi alipata ajali ya gari huko Mpanda Rukwa akapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu na kutokana na afya yake kutetereka alikuwa akipatiwa matibabu Bugando, Kenya na India. 


Hata hivyo  kutokana na matibabu  hayo alipata nafuu na kwa nyakati tofauti alikuwa anapata maumivu ya kichwa na mnamo tarehe 3.4.2023 akiwa jijini Mwanza aliugua ghafla jijini akafariki dunia.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Musoma Food, Said Kate Makilagi alizaliwa 01.06.1967 alifariki dunia 03.04.2023, ameacha mjane na watoto wawili.

Tazama matukio katika Picha ...Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Soma pia :


Shuhudia Hapa : MAZISHI YA MFANYABIASHARA MAARUFU MUSOMA FOOD

Mazishi ya mwili wa Mfanyabiashara wa nafaka mkoa wa Shinyanga/Mkurugenzi wa Kampuni ya Musoma Food…Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post