MAMA AMCHINJA BINTI YAKE KISHA KUMLA


Mwanamke mmoja mtaani Kitengela kaunti ya Kajiado nchini Kenya amewaacha wakaazi wa eneo hilo vinywa wazi kwa kumchinja kwa kisu binti yake kisha kula viungo vyake vya ndani.

Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 24 na mwanafunzi wa chuo kikuu alimchinja binti yake wa miaka miwili na kuanza "kuzungumza kwa ndimi".

Majirani wanasema kuwa walisikia kilio cha kutaka msaada cha mtoto huyo na walipofika walikuta shingo yake ikiwa imekatwa na viungo vya ndani kuliwa na mamake.

Polisi wanasema kuwa walifika eneo hilo mtoto huyo akiwa tayari amefariki na mamake akiwa amezirai kutokana na kipigo alichopewa na majirani.

Dada huyo ambaye kwa sasa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kitengela alisema kuwa alitekeleza unyama huo kwa sababu anajichukia. 

"Mwenyenwe binafsi, ninajichukia. Sijipendi na ndiposa nikamuua binti. Nimepitia hali ngumu na huyu mtoto," mshukiwa amenukuliwa na Taifa Leo.


Chanzo - Tuko news

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post