PASTA AZUA GUMZO AKIMLAZIMISHA MUUMINI KULIA KWA NGUVU KUTHIBITISHA MAPEPO YAMETOKA

Video inasambaa ikionesha mbinu ya kipekee na ya kustaajabisha ya mhubiri mwanamke kutoa pepo.

Mchungaji akimfanyia mwanamke maombi maalum ili kuwa na mahusiano yatakayomwezesha kuingia katika ndoa.

 Akiwa katikati ya maombi hayo, alisikika akimtaka mwanamke anayeombewa kupiga kelele ili kuthibitisha kuwa mapepo yaliyokuwa  yanamzuia kuolewa yalikuwa yakimtoka.

Mchungaji huyo alinaswa kwenye video akimwekea mikono mwanamke huyo na kuamuru mapepo yaondoke kwenye mwili wake. Walakini, alisahau kuwa maikrofoni yake ilikuwa imewashwa.

"Tumuombee kwa ajili ya mahaba ili huyu dada tucheze harusi yake," alisema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post