Tazama Picha : RC CHRISTINA MNDEME AWAFUTURISHA WANANCHI SHINYANGA..."TUSIKUBALI WATOTO KULELEWA NA TV, MITANDAO YA KIJAMII"

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewafuturisha wananchi wa Mkoa wa Shinyanga huku akitoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kukemea mmomonyoko wa maadili katika jamii sambamba na kuitaka jamii kuepuka kuwaacha watoto kulelewa na mitandao ya kijamii na Televisheni.

Mkuu huyo wa mkoa ameandaa Futari (Iftar) leo Jumatano Aprili 12,2023 iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislamu, Kikristo, waumini wa dini ya kiislamu, viongozi wa serikali, siasa na wananchi wa mkoa wa Shinyanga.

Mndeme amesema ni wajibu wa kila mzazi na mlezi kuhakikisha anachukua hatua katika malezi ya watoto ili kupunguza vitendo vya uhalifu katika jamii.

“Tusiache watoto walelewe na Tv, tusiache watoto walelewe na mitandao ya kijamii kwani huko wanaiga  tabia zilizo kinyume na maadili yetu matokeo yake kusababisha mmomonyoko wa maadili. Malezi ya watoto yaanzie katika ngazi ya familia. Kila mmoja akitimiza wajibu wake uhalifu utapungua katika jamii”, amesema Mhe. Mndeme.

“Tusichoke kuiombea nchi yetu, tuombe umoja na mshikamano wetu uendelee kudumu kwani tumetulia kwa sababu kuna amani na utulivu. Tusichoke kuwaombea viongozi wa serikali na tusichoke kuziombea familia zetu na kamwe tusichoke kukemea mmomonyoko wa maadili na tufanye kazi kazi”,ameongeza.

Aidha amekemea tabia ya kuiga tamaduni zisizofaaa ili kuepuka mmomonyoko wa maadili na kuomba viongozi wa dini kukemea vitendo hivyo.
Viongozi wa Dini ya Kiislamu na Kikristo wakiwa kwenye Hafla ya Futari

Katika hatua nyingine Mndeme amewaomba viongozi wa dini na jamii kwa ujumla kuendelea kuwaombea na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu katika jamii.

Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inatambua na kuthamini mchango wa viongozi wa dini hivyo kuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini katika nyanja mbalimbali.

Hata hivyo amesema serikali itaendelea kushirikiana na wananchi kuleta maendeleo pamoja na kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya amemshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa kuandaa Iftar hiyo akisema ni jambo jema lenye Baraka huku akimuombea dua pamoja na viongozi wengine wa Serikali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Kitendo alichokifanya Mkuu Mkoa kwa kufuturisha waumini wa dini ya kiislamu ni kikubwa dhawabu yake atalipwa na Mwenyezi Mungu na atamzidishia zaidi ya alichotoa.Sisi viongozi wa dini tutaendelea kuliombea amani Taifa, pamoja na kumuombea na Afya njema Mheshimiwa Rais Samia na Serikali yake yote ili aendelee kuliongoza vyema Taifa na kuwaletea maendeleo Watanzania",amesema Sheikh Makusanya.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akizungumza na kuomba dua wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo Jumatano Aprili 12,2023

Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategire akizungumza na kuomba dua wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo Jumatano Aprili 12,2023
Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategire akizungumza na kuomba dua wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo Jumatano Aprili 12,2023
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akitoa neno wakati wa Hafla ya Futari aliyoiandaa kwa ajili ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Aprili 12,2023

Sheikh Majaliwa akizungumza na kuomba dua wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo Jumatano Aprili 12,2023
Sheikh Majaliwa akizungumza na kuomba dua wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo Jumatano Aprili 12,2023
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo Jumatano Aprili 12,2023

Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategire akiongoza Swala ya saa 1 usiku nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya na viongozi mbalimbali wakipata Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo Jumatano Aprili 12,2023
Viongozi wa dini ya Kiislamu wakipata Futari
Viongozi wa dini ya Kiislamu wakipata Futari
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akipata chakula
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akipata chakula
Viongozi wa dini ya Kiislamu wakipata Futari
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu (kushoto) akiteta jambo na Askofu Mstaafu wa kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Joseph Makala wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme. Wa Kwanza kulia ni Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Kategire akifuatiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Bin Khamis
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi (kushoto) , akiwa na waumini wa dini ya Kiislamu wakipata chakula

Waumini wa dini ya Kiislamu na wananchi wa Shinyanga wakiwa nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments