Tazama Picha : SWALA YA EID -EL -FITR SHINYANGA....SHEIKH MAKUSANYA ATOA KAULI NZITO CCM NA VYAMA VYA UPINZANI

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akitoa Ujumbe wa Sikukuu ya Eid El Fitr baada ya Ibada ya Eid El Fitri katika uwanja wa Saba Saba Mjini Shinyanga 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya amewataka Watanzania kupendana (Waislamu na wasiokuwa Waislamu, Wenye dini na wasiokuwa na dini) huku akitaka vyama vya upinzani na chama tawala (CCM) vipendane, visogezane, visaidiane kwa ajili ya kuitengeneza nchi ya Tanzania akisisitiza kuwa kama hakuna vyama pinzani basi harakati ya maendeleo itakuwa ni ndogo.

Sheikh Makusanya ameyasema hayo leo Jumamosi Aprili 22,2023 wakati akitoa Ujumbe wa Sikukuu ya Eid El Fitr baada ya Ibada ya Eid El Fitri katika uwanja wa Saba Saba Mjini Shinyanga.

“Tunamuombea Rais Samia Suluhu Hassan pamoja serikali yake pamoja na chama chake lakini pia tunaviombea na vyama pinzani kwa sababu kama hakuna vyama pinzani basi harakati ya maendeleo itakuwa ni ndogo na wao tunawaombea Mwenyezi Mungu awape kila la heri. Hawa vyama vya upinzani hawa na chama tawala vipendane, visogezane,visaidiane kwa ajili ya kuitengeneza nchi ya Tanzania”,amesema Sheikh Makusanya.

Ibada ya Eid El Fitr ikiendelea katika uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga

“Tunamuomba Mwenyezi Mungu kwa kufunga kwetu siku 30, kwa kusimama kwetu, misimamo mbalimbali ya ibada mbalimbali, Mwenyezi Mungu atuletee amani na utulivu katika nchi yetu ya Tanzania. Mwenyezi Mungu atuletee kupendana Waislamu na wasiokuwa Waislamu, Wenye dini na wasiokuwa na dini. Tunamuomba Mwenyezi Mungu kwa visimamo hivi na swaumu hizi, Mwenyezi amkurubie muda wa uongozi wake, Rais wetu kipenzi cha watu, mwenye huruma na watu asiyetaka makuu, kila mwananchi ni wa kwake, habagui, Mwenyezi Mungu ampe kila la heri.

Na kila yeyote aliyepewa dhamana ama na Mwenyezi Mungu, ama na Rais wetu akafanye hiyana katika dhamana yake aliyopewa, Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtu huyu amfichue, afichuke ili watu wamuelewe kwamba anafanya hiyana, anawafanyia hiyana Watanzania na yeyote yule atakayeonesha dhuluma ya kuidhulumu Tanzania, ya kumdhulumu Rais wetu tunakukabidhi kwako wewe Mwenyezi Mungu”,amesema Sheikh Makusanya.

Akitoa hotuba wakati wa Swala ya Eid Elf Fitri, Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Kategire amesema baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani matendo mema yaendelee kufanywa na waumini wa dini ya kiislamu badala ya kurudi kwenye uovu.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akitoa Ujumbe wa Sikukuu ya Eid El Fitr baada ya Ibada ya Eid El Fitri katika uwanja wa Saba Saba Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akitoa Ujumbe wa Sikukuu ya Eid El Fitr baada ya Ibada ya Eid El Fitri katika uwanja wa Saba Saba Mjini Shinyanga 
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akitoa Ujumbe wa Sikukuu ya Eid El Fitr baada ya Ibada ya Eid El Fitri katika uwanja wa Saba Saba Mjini Shinyanga 
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akitoa Ujumbe wa Sikukuu ya Eid El Fitr baada ya Ibada ya Eid El Fitri katika uwanja wa Saba Saba Mjini Shinyanga 
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akitoa Ujumbe wa Sikukuu ya Eid El Fitr baada ya Ibada ya Eid El Fitri katika uwanja wa Saba Saba Mjini Shinyanga 
Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Kategire akitoa hotuba wakati wa Ibada ya Eid El Fitri katika uwanja wa Saba Saba Mjini Shinyanga 

Ibada ya Eid El Fitri ikiendelea katika uwanja wa Saba Saba Mjini Shinyanga

Sheikh Salum Khamis akiongoza Ibada ya Eid El Fitri katika Msikiti wa Safina Ndembezi Mjini Shinyanga

Ibada ya Eid El Fitri ikiendelea katika Msikiti wa Safina Ndembezi Mjini Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde  - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments