AUAWA KWA KUCHOMWA KISU TUMBONI


Charles Elias (18) Mkazi wa Mtaa wa Kigoma, mkoani Katavi amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu tumboni na watu wasiojulikana majira ya usiku katika eneo la Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Ali Makame amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa uchunguzi unaendelea.

Naye Mama wa kijana huyo aliyepoteza maisha Easter Helman ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo limesababisha kifo cha mtoto wake na kuliomba jeshi la polisi kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika.

Tukio hilo linajiri ikiwa ni wiki moja imepita baada ya kutokea tukio lingine la kuuawa kwa kijana Michael Chapa mkazi wa Shanwe, kwa kile kilichodaiwa kujihusisha na vikundi vya uhalifu maarufu kama Damu Chafu.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments