WMA YAPONGEZWA NA KAMATI YA KILIMO, BIASHARA NA UTALII BARAZA LA UWAKILISHI ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar Mhe. Yusuph Hassan Iddi akiongozana na Wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu mkoani Pwani leo Machi 6,2023.

*********************

Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar imeipongeza taasisi ya Wakala wa Vipimo kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake katika kuhakikisha inawalinda watumiaji wa vipimo mbalimbali.

Akizunguamza mara baada ya kufanya ziara ya kujifunza kwenye kituo cha uhakiki cha Wakala wa Vipimo kilichopo Misugusugu Mkoa wa Pwani Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Yusuph Hassan Iddi amesema, kupitia ziara hii wamejifunza mambo mengi kwakuwa na wao upande wa Zanzibar wana taasisi kama hii ambayo inaitwa ZAWEMA japo kwa upande wa Tanzania bara ilianza muda tangu mwaka 2002 hivyo kuna mengi ya kujifunza ili kuweza kuishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuiwezesha taasisi yake ya Vipimo katika kusimamia usahihi wa vipimo kwenye maeneo mbalimbali.

Mhe. Yusuph ameeleza kuwa taasisi hizi za vipimo ni muhimu sana kwa kuwa zihahakikisha zinamlinda mtumiaji wa mwisho wa vipimo kupata vipimo sahihi ndiomana hata kwenye sekta ya afya mgonjwa anapimwa kwanza uzito ili apate dozi inayoendana na uzito wake kwakuwa kinyume na kufanya hivyo anaweza pata madhara. Kadhalika, kwenye usalama wakala wa Vipimo inajukumu la kuhakiki tochi za maafisa wa usalama barabarani ili kujiridhisha kama zinafanya kazi kwa usahihi lakini pia kwenye biashara taasisi hizi za vipimo zinasaidia kuhakikisha Mwananchi anapata bidhaa kwa usahihi kulingana na thamani ya fedha anayotoa bila kupunjwa.

Mhe. Yusuph amesema kamati inaipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiwezesha Wakala wa Vipimo kujenga kituo kikubwa na cha kisasa ambacho kinafanya shughuli za upimaji wa matenki ya malori ya kusafirisha mafuta, lakini pia, wamemeona mitambo ya kisasa ambayo inatumika kupima mita za maji na umeme kabla hazijaenda kufungwa kwa wateja na upimaji huu utasaidia sana kupunguza malalamiko kwa Wananchi wanaotumia huduma hizo ndio maana kama kamati tutashauri ili na upande wa Zanzibar tuweze kupata kituo cha aina hii ili kuwalinda watumiaji wa huduma hizo.

Kwa upande wake Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) ameishukuru na kuipongeza kamati kwa kutembelea taasisi ya Wakala wa Vipimo katika kituo chake cha Upimaji Misugusugu kwa ziara ya kujifunza kazi zinazofanywa na taasisi hiyo ambapo wametembezwa na kushuhudia kazi mbalimbali zinavyofanyika ikiwa ni pamoja na upimaji wa matenki ya malori ya kusafirisha mafuta, upimaji wa mita za umeme pamoja na Dira za Maji.

Ameeleza kuwa kupitia ziara hii anaamini watajifunza mambo mengi lakini pia ni fursa ya kubadilishana mawazo ya namna ya kuboresha taasisi hizi na wamepokea ushauri uliotolewa na Kamati hasa kwenye eneo la kuweka alama kwenye dip stick kutumika njia za kisasa zaidi kuliko zinazotumika kwa sasa.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu akizungumza na waandishi ameeleza kuwa ushirikiano baina ya Wakala wa Vipimo Zanzibar (ZAWEMA) na Wakala wa Vipimo Tanzania Bara (WMA) umeanza muda kwa kushirikiana kubadilishana uwezo wa kitaalamu na vitendea kazi ili kuhakikisha Wananchi wanapata bidhaa zenye vipimo sahihi. Pia, taasisi hizi zinashirikiana hata katika suala la kutoa elimu kwenye maonesho mbalimbali kama ya Mapinduzi na elimu ya vipimo kwa Wafanyabiashara mbalimbali kama masonara wanaouza vito na madini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo Zanzibar (ZAWEMA) Bw. Mohamed Simai ameishukuru Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii ya Baraza la Uwakilishi Zanzibar kwa kutenga muda kuja kujifunza namna shughuli za vipimo zinavyofanyika kwakuwa anaamini itawasaidia katika kuweza kuishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuiwezesha zaidi ZAWEMA ili iweze kutanua wigo wa utekelezaji wa majukumu yake na kuhakikisha inawalinda Wananchi katika sekta mbalimbali kwa kusimamia matumizi ya Vipimo sahihi. Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar Mhe. Yusuph Hassan Iddi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati hiyo kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu mkoani Pwani leo Machi 6,2023.

Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu mkoani Pwani leo Machi 6,2023.


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA) Bi.Stella Kahwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu mkoani Pwani leo Machi 6,2023.Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Vipimo Zanzibar Bw.Muhamed Simai akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu mkoani Pwani leo Machi 6,2023.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar Mhe. Yusuph Hassan Iddi akiwa na Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe wakipata picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo na watumishi wa WMA mara baada ya Kamati hiyo kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu mkoani Pwani leo Machi 6,2023.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii Baraza la Uwakilishi Zanzibar Mhe. Yusuph Hassan Iddi akipongezana na Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe mara baada ya Kamati hiyo kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu mkoani Pwani leo Machi 6,2023.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post