LEAT WATOA MAFUNZO YA MFUMO WA UFUATILIAJI WA UWAJIBIKAJI JAMII NA UTAWALA BORA KWA WATENDAJI WA KATA NA MABARAZA YA KATA BUTIAMA

 

Timu ya wanasheria watetezi wa mazingira kwa vitendo (LEAT) wakitoa mafunzo ya mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Butiama.

Na Marco Maduhu, BUTIAMA

TIMU ya wanasheria watetezi wa mazingira kwa vitendo, Lawyers Environment Action Team (LEAT), wametoa mafunzo ya mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Mafunzo hayo yameanza kutolewa leo Machi 27, 2023 ambayo yatakwenda muda wa siku tano hadi Machi 31 mwaka huu, kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao namna ya kusimamia Rasilimali za nchi na utunzaji wa mazingira.

Mkufunzi wa mafunzo hayo Hana Lupembe kutoka (LEAT), amesema viongozi hao wakipewa elimu hiyo ya mfumo wa ufuatilijai wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora itawasaidia katika utendaji wao kazi kwa wananchi na kufanya vyema katika usimamizi wa Rasilimali za nchi na kuzuia uharibifu wa mazingira katika uchimbaji madini.

“Mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii ni dhana Shirikishi inayohusisha watoa huduma na wapokea huduma kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu, na mfumo huu ukifuatwa vizuri kutakuwa na uwajibikaji kwa viongozi, kutoa huduma bora, kuwa waadilifu na wawazi,”amesema Lupembe.

Aidha, ametaja hatua tano za mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii kuwa ni Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali, usimamizi wa matumizi, usimamizi wa utendaji, usimamizi wa uadilifu, na usimamizi wa uangalizi.

Naye Valeria Macha kutoka (LEAT) amesema licha ya kutoa mafunzo ua utunzaji wa mazingira pia wanawajengea uwezo wananchi na viongozi wanaoishi katika maeneo ya uchimbaji wa madini kujua haki zao za msingi pamoja na kurudisha uoto wa asili baada ya uchimbaji na kuhamia eneo jingine ili kuzuia uharibifu wa mazingira.

Kwa upande wake Afisa usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira wilaya ya Butiama Karani Ruhumbika, amewataka viongozi hao kila mmoja katika eneo lake awe na wajibu wa kutunza mazingira pamoja na wananchi kufanya uchimbaji wa madini uwe salama bila ya kuathiri mazingira.

Nao baadhi ya Watendaji wa Kata Wilaya ya Butiama ambao wanatoka kwenye maeneo ya uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu, wamesema mafunzo hayo yatakuwa chachu ya uongozi wao na kuongeza uwajibikaji katika majukumu yao pamoja na kusimamia vyema rasilimali za taifa na utunzaji wa mazingira.
Mkufunzi wa mafunzo Hana Lupembe kutoka (LEAT) akitoa mafunzo hayo kwa Watendaji wa Kata na viongozi wa Mabaraza ya Kata kutoka wilaya ya Butiama.
Mkufunzi wa mafunzo Hana Lupembe kutoka (LEAT) akitoa mafunzo hayo kwa Watendaji wa Kata na viongozi wa Mabaraza ya Kata kutoka wilaya ya Butiama.
Valeria Macha kutoka (LEAT) akitoa mafunzo kwa viongozi hao Watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Valeria Macha kutoka (LEAT) akitoa mafunzo kwa viongozi hao Watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Afisa usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira wilaya ya Butiama Karani Ruhumbika akitoa mafunzo kwa watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata wilayani Butiama mkoani Mara.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post