JUKWAA LA MAENDELEO YA USHIRIKA 2023 LAFANYIKA MKOANI SHINYANGA

 

Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

JUKWAA la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga, limefanyika leo kwa kujadili changamoto mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi ili kuviimarisha vyama vya ushirika mkoani Shinyanga.

Jukwaa hilo limefanyika leo Marchi 6, 2023, Katika Chuo cha Ushirika Moshi (MocU) Tawi la Kizumbi Manispaa ya Shinyanga, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Kaimu Naibu Mrajisi Uratibu na Uhamasishaji Tume ya Maendeleo na Ushirika Tanzania (TCDC) Consolata Kiluma.

Kiluma akizungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa hilo, amempongeza Rais Samia, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuunga mkono Sekta ya Kilimo, pamoja na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, kwa kazi kubwa ambayo anifanya hasa kwenye kuimarisha vyama vya ushirika ambavyo ndiyo mkombozi wa Mkulima.

Amesema Ushirika kwa sasa unafanya vizuri tofauti na miaka mitatu iliyopita, kutokana na viongozi wakubwa kuunga mkono eneo la kilimo, pamoja na kuwa nao bega kwa bega kuwasimamia na kuwajenga ili kuhakikisha Ushirika unaendelea kusimama imara.

“Katika kuendelea kuimarisha vyama vya Ushirika mkoani Shinyanga napenda kusisitiza mambo machache, viongozi wa vya vyama vya Ushirika mnachangamoto ya kutofuata Sheria ya vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013, pamoja na Kanuni zake za mwaka 2015 na Sheria ya huduma ndogo ya fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019,”anasema Kiluma.

“Viongozi mkifuata Sheria hizi mtaendelea kuimarisha vyama vya ushirika, pia mnapaswa kuwa waadilifu, waaminifu ili kurudisha Taswira nzuri ya vyama vya Ushirika, pamoja na kutangaza mambo mazuri ambayo mnayafanya ndani ya jamii,”ameongeza.

Aidha, amesema Jambo jingine ambalo linapaswa kufanyiwa kazi na viongozi wa vyama vya Ushirika, ni kujibu hoja za Mkaguzi kutoka kwa Mkaguzi wa vyama vya Ushirika (COASCO) ili vyama vipate Hati Safi.

Katika hatua nyingine amesisitiza viongozi wa vyama vya Ushirika, kufuata taratibu za malipo kwa wakulima hasa pale wanapouza mazao yao, kwa kuwalipa kwa wakati, pamoja na kuongeza thamani ya mazao.

Naye Mkaguzi wa vyama vya Ushirika mkoani Shinyanga (COASCO)Rodrick Kilemile, amesema katika ukaguzi ambao wameufanya mwaka (2021-2022) kwa vyama vya Ushirika 237, vyama vilivyopata Hati safi ni Saba, Shaka 51, isiyoridhisha Tatu, na Hati chafu 176.

Kwa upande wake Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoani Shinyanga Hilda Boniphace, amesema mikakati ambayo wamejiwekea katika msimu ujayo ni kuhakikisha vyama vya Ushirika zaidi ya 153 vinapata Hati safi.

Amesema katika ukuguzi ambao wameufanya kwenye vyama vya Ushirika 81, ambapo vyama 45 ni vya mazao, Sita vya Akiba na Mikopo na huo ni ukaguzi wa mara kwa mara, na ukaguzi maalumu wameufanya kwa vya Sita, na kubaini tatizo la kutozingatiwa makisio yaliyoidhinishwa na Mrajisi, Bodi kukaa Madarakani muda unaopita kiasi, uandishi mbovu wa vitabu, na kukosekana kwa vitabu vya fedha.

“Changamoto ambayo tumeibaini kwenye upatikanaji wa Hati za Mashaka 153 kutoka kwenye vyama vya mazao, ni kutofuta madeni ya nyuma, na tumejipanga dosari zote hizi tunaziondoa kwa kufuta madeni ili tutoke kwenye Hati ya Mashaka na kupata Hati Safi zaidi ya 153,”amesema Boniphace.

Pia ametaja baadhi ya changamoto ambazo zinakabili Ushirika Mkoa wa Shinyanga, ni uzalishaji mdogo vya vya mazao kwamba vyama vinazalisha kilo 300, uongozi kutofuata misingi ya utawala bora, kufanya kazi kimazoea, mipasuko kwenye Bodi na kuvuruga wana Ushirika, pamoja na kuacha kusimamia malengo yaliyokusidiwa kusajili chama, pamoja na watendaji kukosa Sifa na weledi.

Ametaja baadhi ya mafaniko kuwa ni kukagua vyama vya Ushirika 81, ambapo malengo ilikuwa ni kukagua vyama 50 kutoka vya 200 vya mkoa mzima, na wanakabiliwa na upungufu wa Maofisa Ushirika kwamba kwa Mkoa mzima wapo Nane na walipaswa wawe 20.

Amesema pia wametoa mafunzo kwa viongozi 450 na watendaji 174, na kutekeleza mfumo wa uuzaji wa mazao na kuvisajili vyama 261, na kuingiza kwenye mfumo makisio ya vyama 13 vya akiba na mikopo, pamoja na kuendelea kutekeleza miongozo iliyotolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika.

Jukwaa hilo limeendana Sambamba utoaji wa Tuzo kwa vyama vya Ushirika vilivyofanya vizuri, pamoja kumpatia Tuzo ya Heshima Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani kutokana na Mchango Mkubwa alionao kwenye Ushirika.

Kaimu Naibu Mrajisi Uratibu na Uhamasishaji Tume ya Maendeleo na Ushirika Tanzania (TCDC) Consolata Kiluma akizungumza kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga.

Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoani Shinyanga Hilda Boniphace akizungumza kwenye Jukwaa hilo.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha Ushirika Kahama( KACU) Hamisi Majogoro akizungumza kwenye Jukwaa hilo.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU)Kwiyolecha Nkilijiwa akizungumza kwenye Jukwaa hilo.

Katibu Tawala Masaidizi Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata akizungumza kwenye Jukwaa hilo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye Jukwaa hilo.

Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye Jukwaa hilo.

Mkaguzi wa vyama vya Ushirika mkoani Shinyanga (COASCO)Rodrick Kilemile akizungumza kwenye Jukwaa hilo.

Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga mwaka 2023.

Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga mwaka 2023.

Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga mwaka 2023.

Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga mwaka 2023.

Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga mwaka 2023.

Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga mwaka 2023.
Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga mwaka 2023.

Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga mwaka 2023.

Wajumbe wakiwa kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga mwaka 2023.

Kaimu Naibu Mrajisi Uratibu na Uhamasishaji Tume ya Maendeleo na Ushirika Tanzania (TCDC) Consolata Kiluma (kushoto) akitoa Tuzo ya heshima kwa Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani kutoka na mchango wake mkubwa kwenye Ushirika.

Kaimu Naibu Mrajisi Uratibu na Uhamasishaji Tume ya Maendeleo na Ushirika Tanzania (TCDC) Consolata Kiluma (kushoto) akitoa Tuzo kwa Chama Kikuu Cha Ushirika Kahama (KACU) kutokana na kufanya vizuri kwenye Ushirika (kulia) ni Mwenyekiti wa KACU Hamis Majogoro

Kaimu Naibu Mrajisi Uratibu na Uhamasishaji Tume ya Maendeleo na Ushirika Tanzania (TCDC) Consolata Kiluma (kushoto) akitoa TUZO kwa SACCOS ya UDIDA.

Tuzo zikiendelea kutolewa.

Tuzo zikiendelea kutolewa.

Picha za pamoja zikipigwa.

Picha za pamoja zikipigwa.

Picha za pamoja zikipigwa.

Picha za pamoja zikipigwa.

Kaimu Naibu Mrajisi Uratibu na Uhamasishaji Tume ya Maendeleo na Ushirika Tanzania (TCDC) Consolata Kiluma (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoani Shinyanga Hilda Boniphace.

Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoani Shinyanga Hilda Boniphace (kushoto) akipokea Zawadi ya Mchele Kilo 100 kutoka na kuandaa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Shinyanga na Kujadili Changamoto Mbalimbali za Ushirika na kuzitafutia ufumbuzi ili kuimarisha Ushirika.

Awali wana Ushirika wakiwa katika maandamano ya kuelekea kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika katika Chuo cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi.

Awali wana Ushirika wakiwa katika maandamano ya kuelekea kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika katika Chuo cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments