VIJANA WAWILI WALIOMUUA MAMA YAO WA KAMBO WAUAWA


Mkuu wa wilaya ya Geita akiwa na Jeshi la Polisi pamoja na wanafamilia

Vijana wawili wa familia moja wakazi wa kitongoji cha Kilimahewa kata ya Ludete mkoani Geita, wameuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumuua mama yao wa kambo Renatha Elias alikuwa mjamzito wa miezi saba kwa kumkata shingo.


Baadhi ya ndugu na shuhuda wa tukio hilo wanaelezea jinsi Watoto hao walivyoingia kwenye nyumba na kuanza kumpiga sehemu mbalimbali na kumkata kichwa mama huyo aliekuwa mjamzito.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Kilimahewa anasema waliotekeleza mauaji hayo ni Watoto wa baba mwenye mji kwa mama mwingine ambao pia walimjeruhi baba yao kwa kumchoma na visu ambae kwa sasa yupo hospital anapatiwa matibabu.

Chanzo - EATV

Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe amefika katika tukio hilo na kuzungumza na wafiwa pamoja na waombolezaji huku akikemea mauaji ya kinyama na kuliagiza Jeshi la Polisi kudhibiti matukio ya mauaji na ujambazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments